\v 5 Yehoakimu alikuwa na umri wa miaka ishini na tano alipoanza kutawala, na akatawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Akafanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe Mungu wake. \v 6 Kisha Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akamvamia na kumfunga katika minyororo kumuongoza kwenda mbali Babeli. \v 7 Nebukadreza pia akabeba baadhi ya vitu katika nyumba ya Yahwe kwenda Babeli, na akaviweka katika ikulu yake huko Babeli.