\v 21 Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na mbili alipoanza kutawala; alitawala miaka miwili katika Yerusalemu. \v 22 Akafanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe, kama Manase, baba yake, alivyofanya. Amoni alitoa sadaka katika sanamu zote za kuchonga ambazo alitengeneza Manase baba yake, na aliziabudu. \v 23 Hakujinyenyekesha mbele za Yahwe, kama baba yake Manase alivyokuwa amefanya. Badala yake, Amoni alifanya makosa zaidi na zaidi.