sw_1th_text_ulb/02/10.txt

1 line
382 B
Plaintext

\v 10 Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, ni kwa utakatifu wa namna gani, haki, na bila lawama tulivyoenenda wenyewe mbele yenu mnaoamini. \v 11 Vivyo hivyo, mnajua ni kwa namna gani kwa kila mmoja wenu, kama baba alivyo kwa wanawe tulivyowahimiza na kuwatia moyo. Tulishuhudia \v 12 kwamba mlipaswa kuenenda kama ulivyo mwito wenu kwa Mungu, aliyewaita kwenye ufalme na utukufu wake.