sw_1sa_text_reg/19/18.txt

1 line
453 B
Plaintext

\v 18 Basi Daudi akakimbia na kutoroka, na akaenda kwa Samweli huko Rama na kumweleza yote ambayo Sauli amemtendea. Ndipo yeye na Samweli wakaenda na kukaa Nayothi. \v 19 Naye Sauli akaambiwa kwamba, "Tazama, Daudi yuko huko Nayothi iliyoko Rama." \v 20 Kisha Sauli akawatuma wajumbe kumkamata Daudi. Nao walipowaona kundi la manabii wakitabiri, na Samweli akisimama kama kiongozi wao, Roho wa Mungu akawaingia wale wajumbe wa Sauli, nao pia wakatabiri.