sw_1sa_text_reg/17/19.txt

1 line
414 B
Plaintext

\v 19 Kaka zako wako pamoja na Sauli na watu wote wa Israeli katika bonde la Ela, wanapigana na Wafilisti." \v 20 Daudi aliamka asubuhi na mapema na kuliacha kundi chini ya uangalizi wa mchungaji. Akachukua vile vitu na kuondoka, kama Yese alivyomwamuru. Akafika kambini wakati jeshi linaondoka kwenda uwanja wa vita wakipiga kelele za vita. \v 21 Nao Israeli na Wafilisti walijipanga kivita, jeshi dhidi ya jeshi.