\v 31 Maneno aliyosema Daudi yaliposikika, askari waliyasema tena kwa Sauli, naye akawatuma kwa Daudi. \v 32 Kisha Daudi akamwambia Sauli, "Pasiwepo moyo wa mtu utakayezimia kwa sababu ya Mfilisti huyo; Mtumishi wako atakwenda kupigana na Mfilisti huyu." \v 33 Sauli akamwambia Daudi, "Huwezi kumpinga Mfilisti ama kupigana naye; wewe ni kijana tu, na yeye amekuwa mtu wa vita tangu ujana wake."