sw_1ki_text_reg/08/54.txt

1 line
484 B
Plaintext

\v 54 Kwa hiyo ilitokea wakati Sulemani alipomaliza kuomba maombi haya na dua zake kwa BWANA, aliamka toka madhabahu ya BWANA, pale alipokuwa amepiga magoti na mikono yake ikiwa imenyoshwa kuelekea mbinguni. \v 55 Alisimama na kuubariki mkutano wote wa Israeli kwa sauti kuu, alisema, \v 56 "Asifiwe BWANA, aliyewapatia pumziko watu hawa Israeli, akitunza ahadi zake zote. Hakuna hata moja ambayo haijatekelezwa katika ahadi njema za BWANA ambazo aliahidi akiwa na Musa mtumishi wake.