sw_1ki_text_reg/02/01.txt

1 line
710 B
Plaintext

\c 2 \v 1 Daudi alipokaribia kufa, alimwamuru Sulemani mwanae, akisema, \v 2 "Mimi sasa ninaiendea njia ya dunia yote. Kwa hiyo, uwe imara, na ujionyeshe mwenyewe kama mwanamume. Uzilinde amri za BWANA, Mungu wako ukitembea katika njia zake, utii maaagizo yake, amari zake, \v 3 maamuzi yake, na maagizo ya maagano yake, uwe mwangalifu kufanya yale yaliyoandikwa katika sheria za Musa, ili ufanikiwe katika yote utakayoyafanya, popote kule utakakokuwa, \v 4 na BWANA atayatimiza maneno yake aliyosema kuhusu mimi, aliposema, 'kama wanao watajilinda katika tabia zao, wakatembea mbele yangu kwa uaminifu kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote, hawatakoma kuwa na mtu aliyeketi katika kiti cha enzi cha Israeli.