Sat Jul 02 2022 11:16:04 GMT+0300 (East Africa Time)

This commit is contained in:
nicholuskombo 2022-07-02 11:16:25 +03:00
commit 0427ad8787
361 changed files with 427 additions and 0 deletions

1
01/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Mfalme Daudi alipokuwa mzee sana, walimfunika kwa nguo, lakini hakupata joto. \v 2 Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, "Na tutafute msichana bikra kwa ajili ya mfalme bwana wetu. Ili amtumikie na kumtunza. Naye atalala kwenye mikono yake ili bwana mfalme wetu apate joto.

1
01/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Kwa hiyo wakatafuta msichana mrembo katika mipaka yote ya Israeli. Wakampata Abishagi Mshunami wakamlte kwa mfalme. \v 4 Yule msichana alikuwa mrembo sana. Naye akamtumikia mfalme na kumtunza, Lakini mfalme hakumjua.

1
01/05.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 5 Wakati huo, Adoniya mwana wa Hagithi alijiinua akisema, "Nitakuwa mfalme." Kwa hiyo akajiandalia magari na wapanda farasi hamsini ili wapige mbio mbele yake. \v 6 Baba yake alikuwa hajawahi kumsumbua, kwa kusema, "kwa nini umefanya hili na lile?" Adoniya allikuwa mwanamume mzuri sana aliyezaliwa baada ya Absalomu.

1
01/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Akashauriana na Yoabu mwana wa Seruya na Abiathari kuhani. Wakamfuata Adoniya wakamsaidia. \v 8 Lakini Sadoki kuhani, Benaya mwana wa Yehoyada, nabii Nathani, Shimei, Rei, na watu mashujaa wa Daudi hawakumfuata Adoniya.

1
01/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Adoniya akataoa dhabihu za Kondoo, na ndama walionona kwenye jiwe la Sohelethi, ambalo liko karibu na Eni Rogeli. Akawakaribisha ndugu zake wote, watoto wa mfalme, wanaume wote wa Yuda, na watumishi wa mfalme. \v 10 Lakini hakumkaribisha nabii Nathan, Benaya, wanaume mashujaa, au ndugu yake Sulemani.

1
01/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Kisha Nathani akamwambia Bethisheba mama wa Sulemani, akaisema, "Je, haujasikia kuwa Adoniya mwana wa Hagathi amekuwa mfalme, na Daudi bwana wetu halijui hilo? \v 12 Kwa hiyo sasa nakupa ushauri, ili kwamba uweze kuokoa maisha yako na maisha ya mwanao Suleimani.

1
01/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Nenda kwa mfalme Daudi; ukamwambie, 'Bwana wangu mfalme, Je, haukumwapia mtumishi wako, ukisema, "Hakika Sulemani mwanao atatawala baada yangu, na ataketi kwenye kiti changu cha enzi?" Kwa nini basi Adoniya anatawala?' \v 14 Wakati ukiwa pale ukiongea na mfalme, Nitaingia baada yako na kuthibitisha hayo.

1
01/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Kwa hiyo Bathisheba akaingia chumbani kwa mfalme. Wakati huo mfalme alikuwa mzee sana, na Abishagi Mshunami alikuwa akimtunza mfalme. \v 16 Bathisheba akaiinama kifudifudi mbele ya mfalme. Na kisha mfalme akasema, "Una haja gani?" \v 17 Naye akamwambia, "Bwana wangu, ulimwapia mtumishi wako kwa jina la BWANA, Mungu wako, ukisema, 'Hakika Sulemani mwanao atatawala, baada yangu, naye ataketi kwenye kiti changu cha enzi.'

1
01/18.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 18 Sasa, tazama, Adoniya ni mfalme, na bwana wangu mfalme hajui jambo hili. \v 19 Ametoa dhabihu ya makisai, ndama walionona, na kondoo wengi, na amewakaribisha wana wote wa mfalme, Abiathari kuhani, na Yoabu jemedari wa jeshi, lakini hajamkaribisha Sulemani mtumishi wako.

1
01/20.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 20 Mfalme bwana wangu, macho yote ya Israeli yako kwako, yakisubiri usemi wako juu ya nani atakayeti kwenye kiti cha enzi baada yako, bwana wangu. \v 21 Vinginevyo itatokea, wakati bwana wangu atakapolala na baba zake, kwamba Mimi na mwanangu Sulemani kuhesabiwa wahaini."

1
01/22.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 22 Wakati alipokuwa akiendelea na mfalme, nabii Nathani aliingia. \v 23 Watumshi wakamwambia mfalme, "Nabii Nathani yuko hapa," Naye alipoingia mbele ya mfalme, akalala kifudifudi mbele ya mfalme na uso wake ukielekea chini.

1
01/24.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 24 Nathani akamwambia, "Mfalme bwana wangu, Je, umesema, Adoniya atatawala baada yangu, na ataketi kwenye kiti changu cha enzi? \v 25 kwani leo ameshuka na ametoa dhabihu ya makisai, ndama walionona, na kondoo wengi, na amewakaribisha wana wote wa mfalme, jemedari wa jeshi, na Abiatahari kuhani. Nao wanakuka na kunywa mbele zake, na kusema, 'Mfalme Adoniya na aishi milele!'

1
01/26.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 26 Lakini mimi, mtumishi wako, Sadoki kuhani, Benaya mwana wa Yehoyada, na mtumishi wako Suleimani, hajatukaribisha. \v 27 Je, bwana wangu mfalme amefanya haya pasipo kutuambia sisi, watumishi wako, ni nani atakayeketi kwenye kiti cha enzi baada yake?"

1
01/28.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 28 Ndipo mfalme Daudi lipojibu na kusema, "Mwiteni Bathisheba arudi." Naye akaja akasimama mbele ya mfalme. \v 29 Mfalme akafanya kiapo akasema, "Kama BWANA aishivyo, ambaye ameniokoa toka tabu zote, \v 30 kama nilivyokuapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli, nikisema, 'Sulemani mwanao atatawala baada yangu, naye ndiye atakayeketi kwenye kiti changu cha enzi, mahali pangu,' Nitafanya hivi leo." \v 31 Kisha Bathisheba akalala kifudifudi na sura yake ikielekea chini mbele ya mfalme akasema, "Bwana wangu mfalme Daudi n a aishi milele!"

1
01/32.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 32 Mflme Daudi akasema, "Niitieni Sadoki kuhani, nabii Nathani na Benaya mwana wa Yehoyada." Nao wakaja mbele ya mfalme. \v 33 Mfalme akawaambia, "Uwachukue watumishi wangu, bwana wako, na umfanye Sulemani mwanangu apande juu ya nyumba yangu mimi na mkamtelemshe mpaka chini Gihoni. \v 34 Na Sadoki kuhani na nabii Nathani wamtawaze awe mfalme wa Israeli na tarumbeta zipigwe, 'Mfalme Suleimani na uishi milele!'

1
01/35.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 35 Kisha njoni mkiwa nyuma yake, naye atakuja na kukaa kwenye kiti changu cha enzi; kwani yeye ndiye atakayekuwa mfalme mahali pangu. Nimemchagua yeye kuwa mtawala wa Israeli na Yuda." \v 36 Benaya mwana wa Yehoyada akamjibu mfalme, akasema, "Na iwe hivyo! Na BWANA, Mungu wa mfalme bwana wangu, alithibitishe hilo. \v 37 Kama vile BWANA alivyokuwa na mfalme bwana wangu na awe na Sulemani hivyo hivyo, na kuifanya enzi yake kuwa kubwa kuliko zaidi ya enzi ya bwana wangu Daudi."

1
01/38.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 38 Kwa hiyo Sadoki kuhani, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, na Wakerethi na Wapelethi wakamfanya Sulemani akapanda juu ya nyumba ya mfalme Daudi; wakamleta Gihoni. \v 39 Naye Sadoki kuhani akachukua pembe lenye mafuta hemani akamtia mafuta Sulemani kisha wakapiga tarumbeta, na watu wote wakasema, 'Mfalme Sulemani na aishi milele!' \v 40 Kisha watu wote wakamfuata, na watu wakapiga zomari wakafurahi furaha kubwa mno, kiasi kwamba dunia ikatetemeka kwa sauti zao.

1
01/41.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 41 Kisha Adoniya na wageni wake waliokuwa pamoja naye wakasikia hayo walipomaliza kula. Yoabu alipozisikia sauti za panda, akasema, "Kwa nini jiji lilko katika hali ya taharuki?" \v 42 Wakati alipokuwa akiongea, Yonatahani mwana wa Abiathari kuhani alifika. Adoniya akamwambia, "Karibu, 'kwa kuwa wewe wastahili kutuletea habari."

1
01/43.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 43 Naye Yonathani akamjibu Adoniya, "Mfalme bwana wetu Daudi amemfanya Sulemani kuwa mfalme. \v 44 Na mfalme amemtuma pamoja naye Sadoki, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, na Wakerethi pamoja na Wapelethi. Wamempandisha Sulemani juu ya nyumba ya mfalme. \v 45 Sadoki kuhani na nabii Nathani wamemtawaza kuwa mfalme kule Gihoni, na wametokea huko wakifurahi, ndiyo maana jiji liko katika taharuki. Na hizi ndizo sauti ulizosikia.

1
01/46.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 46 Pia, Sulemani ameketi kwenye kiti cha enzi cha ufalme. \v 47 Zaidi ya yote, watumishi wa mfalme walikuja kumbariki mfalme bwana wetu Daudi, wakisema, 'Mungu wako na alifanye jina la Sulemani kuwa zuri kuliko jina lako, na kuifanya enzi yako kuwa kubwa kuliko yako.' na mfalme akasujudu mwenyewe kitandani. \v 48 Mfalme pia alisema, 'Abarikiwe BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye amempa mtu kuketi kwenye enzi yangu siku hii ya leo, na kwamba macho yangu yamejionea hilo.'"

1
01/49.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 49 Ndipo wageni wote wa Adoniya walipoogopa sana. Wakasimama na kila mtu akaenda njia yake. \v 50 Pia Adoniya alimwaogopa Sulemani na akasimama, na akaondoka, akachukua pembe la madhabahuni. \v 51 Kisha Sulemani akaambiwa hilo, wakasema, "Tazama, Adoniya amemwogopa mfalme Sulemani, kwa kuwa ameshikilia pembe la madhabahuni, akisema, 'Mfalme Sulemani na aniapie kwanza kuwa hatamwua mtumishi wake kwa upanga.'"

1
01/52.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 52 Sulemani akasema, "Kama atajionyesha kuwa ni mtu wa kweli, hakuna hata unywele mmoja utakaoanguka duniani, bali kama uovu utaonekana kwake, atakufa." \v 53 Kwa hiyo mfalme Sulemani akatuma watu, waliomleta Adoniya kutoka madhabahuni. Naye akaja akapiga magoti kwa Sulemani, na Sulemani akamwambia, "Nenda nyumbani kwako."

1
02/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Daudi alipokaribia kufa, alimwamuru Sulemani mwanae, akisema, \v 2 "Mimi sasa ninaiendea njia ya dunia yote. Kwa hiyo, uwe imara, na ujionyeshe mwenyewe kama mwanamume. Uzilinde amri za BWANA, Mungu wako ukitembea katika njia zake, utii maaagizo yake, amari zake, \v 3 maamuzi yake, na maagizo ya maagano yake, uwe mwamngalifu kufanya yale yaliyoandikwa katika sheria za Musa, ili ufanikiwe katika yote utakayoyafanya, popote kule utakakokuwa, \v 4 na BWANA atayatimiza maneno yake aliyosema kuhusu mimi, aliposema, 'kama wanao watajilinda katika tabia zao, wakatembea mbele yangu kwa uaminifu kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote, hawatakoma kuwa na mtu aliyeketi katika kiti cha enzi cha Israeli.

1
02/05.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 5 Wewe pia wajua kile Yoabu mwana wa Seruya alichonifanyia, na kile alichowafnyia majemedari wa majeshi y a Israeli, kwa Abina mwana wa Neri, na kwa Amasa mwana wa Yetheri, ambaye alimwua. Alimwaga damu vitani wakati wa amani na kuiweka ile damu kwenye mshipi uliokuwa kiunoni mwake na kwenye vile viatu miguuni mwake. \v 6 Mshughulikie Yoabu kwa hekima ambayo umejifunza, lakini usiache mvi zake ziingie kaburini kwa amani.

1
02/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Hata hivyo, uonyeshe utu kwa wana wa Barizilai Mgileadi, na uwaache wawe miongoni mwa wale wanaokula mezani kwako, kwa kuwa walikuja kwangu wakati nilipomkimbia ndugu yangu Absalomu.

1
02/08.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 8 Tazama, Shimei mwana wa Gera yuko pamoja na wewe, Wabenjamini wa Bahurimu, walionilaani kwa laana ya fujo siku niliyoenda kwa Mahanaimu. Shimei alishuka kuja kuniona pale Yorodani, na nikamwapia kwa BWANA, nikisema, 'Sitawaua kwa upanga,' \v 9 Kwa hiyo sasa usimwache aiepuke adhabu. Wewe ni mwenye hekima, na utajua jinsi itakavyokupasa kumtendea. Utakileta hicho kichwa chenye mvi chini kaburini."

1
02/10.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 10 Ndipo Daudi alipolala na mababu zake na alizikwa kwenye mji wa Daudi. \v 11 Siku ambazo Daudi alitwala Israeli zilikuwani miaka arobaini. Alikuwa ametawala kwa miaka saba kule Hebroni na kwa miaka thelethini na tatu kule Yerusalemu. \v 12 Kisha Sulemani akaketi kwenye kiti cha enzi cha baba yake Daudi, na utawala wake ulikuwa imara.

1
02/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Kisha Adoniya mwana wa Hagathi alikuja kwa Bathisheba mama wa Sulemani., Naye akamwuliza, "Je, unakuja kwa amani?" Naye akajiibu. "kwa amani." \v 14 Kisha akasema, "Nina jambo la kukuambia." Naye akajibu, "Sema." \v 15 Adoniya amesema, "Unajua kuwa ufalme ulikuwa wangu, na kwamba Israeli yote ilikuwa inanitegemea mimi kuwa mfalme. Hata hivyo, ufalme umegeuzwa na umekuwa wa ndugu yangu, kwani ulikuwa wake toka kwa BWANA.

1
02/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Sasa nina ombi moja kwako. Usinikatalie."Bathisheba akamwambia, "Sema." \v 17 Naye akamwambia, "Tafadhali mwambie mfalme Sulemani, kwa kuwa hatakukatalia, ili kwamba anipatie Abishagi Mshunami awe mke wangu." \v 18 Bathisheba akamwambia, "Vyema sana, nitamwambia mfalme"

1
02/19.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 19 Kwa hiyo Bathisheba akaenda kumwambia, mfalme Sulemani kwa niaba ya Adoniya. Mfalme akainuka kumlaki na akapiga magoti mbele yake. Kisha akaa kwenye kiti chake cha enzi na kulikuwa na kiti kingine cha enzi kilicholetwa kwa ajili ya mama wa mfalme. Naye akaa mkono wa kuume wa mfalme. \v 20 Ndipo alipomwambia, "Napenda kukuomba ombi moja dogo. Usinikalie." Mfalme, akamjibu, "Mama omba kwa kuwa sitakukatalia." \v 21 Naya akamwambia, "Naomba Abishagi Mshunami apewe Adoniya ndugu yako awe mke wake."

1
02/22.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 22 Mfalme Sulemani akamjibu mama yake, "Kwa nini unamwombea Adoniya huyo Abishagi Mshunami? Kwa nini usimwombee ufalme pia, kwa kuwa ni ndugu yangu mkubwa? - au kwa Abiathari kuhani, au Yoabu mwana wa Seruya?" \v 23 Kisha mfalme Sulemani akaapa kwa BWANA, akisema, "Mungu wangu na anifanyie hivyo, na zaidi pia, kama Adoniya hajayasema haya kinyume na maisha yake.

1
02/24.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 24 Sasa basi kama BWANA aishivyo, ambaye ndiye alinifanya mimi kuwepo na kunipa kiti cha enzi cha Daudi baba yangu, na ambaye amenifanyia nyumba kwa ahadi yake, hakika Adoniya lazima auawe leo." \v 25 Kwa hiyo mfalme Sulemani akamtuma Benaya mwana wa Yehoyada naye akamkuta Adoniya na kumwua.

1
02/26.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 26 Kisha akamwambia Abiathari kuhani, "Nenda kwa Anathothi, kwenye mashamba yako. unastahili kufa, lakini sitakua sasa hivi, kwa sababu ulilbeba sanduku la BWANA mbele ya Daudi baba yangu na kujitabisha kwa namna mbalimbali kama baba yangu alivyopata tabu." \v 27 Kwa hiyo Sulemani akamfukuza Abiathari asiwe kuhani wa BWANA, ili kwamba atimilize maneno ya BWANA, aliyokuwa amesema juu ya nyumba ya Eli.

1
02/28.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 28 Habari hizo zikamfikia Yoabu, Kwani Yoabu alimuunga mkono Adoniya, ingawa hakumuunga mkono Absalomu. Kwa hiyo Yoabu akakimbilia kwenye hema ya BWANA karibu na madhabahu na akabeba pembe za madhabahu. \v 29 Sulemani alipoambiwa kuwa Yoabu amekimbilia kwenye hema ya BWANA na sasa alikuwa karibu na madhabahu. Ndipo Sulemani alipomtuma Benaya mwana wa Yehoyada, akisema, "Nenda, ukamwue."

1
02/30.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 30 Kwa hiyo Benaya akaenda kwenye hema ya BWANA na kumwambia, "Mfalme anasema utoke hemani." Yoabu akamjibu, "Hapana, Nitafia hapa," Kwa hiyo Benaya akarudi kwa mfalme, akasema, "Yoabu amesema atafia kwenye madhabahu," \v 31 Naye mfalme akamwambia, "Kafanye kama alivyosema. Muue na ukamzike, ili kwamba uitoe kwangu na kwenye nyumba ya baba yangu damu ambayo Yoabu alimwaga bila sababu.

1
02/32.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 32 BWANA na amrudishie damu yake kichwani kwake, kwa sababu aliwaua wanaume wawili wasio na hatia na wema kuliko yeye na akawaua kwa upanga, Abineri mwana wa Neri, Jemedari wa Jeshi la Israeli, na Amasa mwana wa Jetheri, jemedari wa jeshi la Yuda, bila baba yangu Daudi kujua. \v 33 Kwa hiyo damu yao na imrudie Yoabu kichwani pake na kwenye vichwa vya uzao wake milele na milele. Lakini kwa Daudi na uzao wake, na nyumba yake, na kwenye kiti chake cha enzi, kuwe na amani ya kudumu kutoka kwa BWANA."

1
02/34.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 34 Kisha Benaya mwana wa Yehoyada akaenda akamvamia Yoabu na kumwua. Alizikwa kwenye nyumba yake kule jangwani. \v 35 Mfalme akamwinua Benaya mwana wa Yehoyada kuwa juu ya jeshi badala yake, na akamweka Sadoki kuhani kwenye nafasi ya Abiatahari.

1
02/36.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 36 Kisha Mfalme akatuma watu kumwita Shimei, na akamwambia, "Kajijengee nyumba kwa ajili yako kule Yerusalemu na ushi huko, na usitoke nje ya Huo mji na kwenda mahali pengine. \v 37 Kwa kuwa siku utakayoenda mahali pengine, na kupita bonde la Kidroni, ujue kwa hakika kuwa utakufa. Damu yako itakuwa juu ya kichwa chako." \v 38 Kwa hiyo Shimei akamwambia mfalme, "Unachosema ni chema. Kama vike mfalme bwana wangu alivyosema, ndivyo ambavyo mtumishi wako atakavyofanya." Kwa hiyo Shimei akaishi Yerusalemu kwa miaka mingi.

1
02/39.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 39 Lakiini mwishoni mwa mwaka wa tatu, watumishi wawili wa Shimei wakakimbilia kwa Akishi mwana wa Maaka, mfalme wa Gathi. Kwa hiyo wakamwambia Shimei, wakisema, "Tazama, watumishi wako wameenda Gathi," \v 40 Kisha Shimei akainuka, akapanda punda wake akaenda kwa Akishi huko Gathi kuwatafuta watumishi wake. Akaenda na akawaleta watumishi wake toka Gathi.

1
02/41.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 41 Sulemani alipoambiwa kuwa Shimei alikuwa ametoka Yerusalemu kwenda Gathi na amerudi, \v 42 mfalme akatuma wito kwa Shimei na kumwambia, "Je, sikukuapisha kwa BWANA na kushuhudia kwako, nikisema, 'Tambua kuwa siku utakayotoka kwenda nje na kwenda mahali popote, hakika utakufa'? Na ukaniambia kuwa unachosema ni chema.'

1
02/43.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 43 Kwa nini basi umeshindwa kulinda kiapo chako kwa BWANA na amri niliyokupa?" \v 44 Pia mfalme akamwambia Shimei, "Unajua katika moyo wako maovu yote uliyofanya kwa baba yangu Daudi. Kwa hiyo BWANA atakurudishia maovu yako kichwani pako.

1
02/45.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 45 Lakini Sulemani atabarikiwa na enzi ya Daudi itaimarika mbele ya BWANA milele." \v 46 Kwa hiyo mfalme akamwamuru Benaya mwana wa Yehoyada kwenda kumwua Shimei. Kwa hiyo ule utawala ulikuwa mwema kwa mkono wa Sulemain.

1
03/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Sulemani akawa na ushirikiano wa kindoa na Farao mfalme wa Misri. Alimwoa binti wa Farao na kumleta katika mji wa Daudi mpaka alipomaliza kujenga nyumba yake, nyumba ya BWANA, na ukuta wa Yerusalemu. \v 2 Watu walikuw wakitoa sadaka kwenye maeneo ya juu, kwa sababu hapakuwa bado na nyumba iliyokuwa imejengwa kwa jina la BWANA. \v 3 Sulemani alionyesha upendo wake kwa BWANA kwa kutembea katika maagizo ya Daudi baba yake, isipokuwa tu alitoa dhabihu na kuchoma uvumba mahali pa juu.

1
03/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 Mfalme akaenda Gibioni kutoa sadaka kule, kwa kuwa hilo ndilo lilikuwa eneo kuu la juu. Sulemani katoa sadaka maelfu katika madhabu hiyo. \v 5 BWANA akaonekana kwa Sulemani huko Gibioni katika ndoto ya usiku; akasema, "Omba! uanataka nikupe nini?"

1
03/06.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 6 Kwa hiyo Sulemani akasema, "umeonyesha uaminifu wa agano mkuu kwa mtumishi wako, Daudi baba yangu, kwa sababu alitembea mbele yako kwa ukweli na uaminifu, katika haki ya moyo na katika unyofu wa moyo. Umetunza kwa ajili yake hili agano kuu kwa uaminifu na umempa mwana wake kuketi kwenye kiti chake cha enzi leo.

1
03/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Na sasa, BWANA, Mungu wangu, umemfanya mtumishi wako kuwa mfalme katika nafasi ya Daudi baba yangu, japo mimi ni mtoto mdogo. Sijui namna ya kuiingia na kutoka. \v 8 Mtumishi wako yuko katikati ya watu wako uliowachagua, kundi kubwa, watu wangi wasiohesabika. \v 9 Kwa hiyo umpe mtumishi wako moyo wa uelewa wa kuwahukumu watu wako. Kwani ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi?"

1
03/10.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 10 Ombi hili la Sulemani likampendeza Bwana. \v 11 Kwa hiyo Mungu akamwambia. "Kwa sababu umeomba jambo hili na haujajiombea maisha marefu au utajiri au uhai wa maadui wako, lakini umeomba ufahamu wa kutambua hukumu ya haki, \v 12 Tazama sasa nitafanya yote uliyoniomba wakati uliponipa ombi lako. Ninakupa moyo wa hekima na ufahamu, kwa kuwa hapajawahi kuwa na mtu wa kuwa kama wewe kabla yako, na hakuna wa kuwa kama wewe atakayeinuka baada yako.

1
03/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Pia ninakupa hata ambayo hujaomba, vyote heshima na utajiri, ili kwamba pasije pakawa na mfalme wa kuwa kama wewe katika siku zako zote. \v 14 Kama utatembea katika njia zangu na kuyatunza maagizo yangu na maagizo yangu, kama alivyofanya baba yako Daudi, ndipo nitakapoziongeza siku zako."

1
03/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Kisha Sulemani alipoamka, na tazama, ilikuwa ndoto. Akaja Yerusalemu na akasimama mbele ya sanduku na agano la Bwana. Akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, na akawafanyia sherehe watumishi wake wote.

1
03/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Kisha wanawake wawili waliokuwa makahaba wakaja mbele ya mfalme wakasimama mbele yake. \v 17 Mwanamke mmoja akasema, "Aa, bwana wangu, mwanamke huyu na mimi tunaishi katika nyumba moja, Nilizaa mtoto tukiwa pamoj na yeye katika nyumba yetu.

1
03/18.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 18 Ikatokea siku ya tatu baada ya kujifungua na yeye akajifungua. Tulikuwa sisi tu. Hapakuwepo na mtu mwingine yeyote katika nyumba yetu, ila sisi tu wawili katika hiyo nyumba. \v 19 Kisha mtoto wa mwanamke huyu akafa wakati wa usiku, kwa sababu alimlalia. \v 20 kwa hiyo akamka wakati huo wa usiku wa manane akamchukua mwanangu toka pembeni yangu, wakati mimi mtumishi wako nilipokuwa usingizini, na akamlaza kwenye kifua chake, na akamlaza mtoto wake aliyekufa juu ya kifua changu.

1
03/21.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 21 Asubuhi nilipoamka ili kumhudumia mwanangu, nikaona kuwa alikuwa amekufa. Lakini nilipomwangalia kwa makini wakati huo wa asubuhi, nikagundua kuwa hakuwa yule mwanangu niliyezaa," \v 22 Yule mwanamke mwingine akasema, "Hapana, Huyu aliye hai ndiye wangu. Na yule aliyekufa ndiye wako." Yule mwanamke wa kwanza akasema, "Hapana, Yule mtoto aliyekufa ndiye mwanao, na huyu aliye hai ndiye wangu." Hivi ndivyo walivyoongea mbele ya mfalme.

1
03/23.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 23 Kisha mfalme akasema, "Mmoja wenu anasema, 'huyu aliye hai ni wangu, na kumbe mwanao ndiye aliye kufa,'na mwingine naye anasema, 'Hapana, mwanao ni yule aliyekufa, na mwanangu ni huyu aliye hai.'" \v 24 Mfalme akasema, ''Nileteeni upanga." Kwa hiyo wakaleta upanga kwa mfalme. \v 25 Kisha mfalme akasema, "Mgawe mtoto aliye hai katika vipande viwili, na huyu mwanamke apewe nusu na yule mwingine naye apewe nusu."

1
03/26.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 26 Yule mwanamke mwenye mtoto aliyekuwa hai akamwambia mfalme, kwa kuwa moyo wake ulikuwa na huruma sana kwa mwanae, akasema, "Aa, bwana wangu, mpatie huyu mtoto aliye hai, na usimwue kamwe." Lakini yule mwanamke mwingine akasema, "Hatakuwa wangu wala wako. Mgawe." \v 27 Ndipo mfalme aliposema, "Mpe yule mwanamke wa kwanza mtoto aliye hai, na kamwe usimwue. Yeye ndiye mama wa mtoto huyu." \v 28 Israeli wote waliposikia hukumu ambayo mafalme ametoa, walimwogopa mfalme, kwa sababu waliona kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake kwa ajili ya kutoa kuhukumu.

1
04/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Mfalme Sulemani alikuwa mfalme wa Israeli. \v 2 Hawa ndio waliokuwa wakuu wake: Azaria mwana wa Sadoki alikuwa kuhani. \v 3 Elihorefu na Ahiya mwana wa Shisha, walikuwa makatibu. Yehoshafati mwana wa Ahilui alikuwa mwandishi. \v 4 Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mkuu wa jeshi. Sadoki na Abiatahari walikuwa makuhani.

1
04/05.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 5 Azaria mwana wa Natahani ndiye aliyekuwa juu ya hawa maakida. Zabudi mwana wa Nathani alikuwa kuhani na rafiki wa mfalme. \v 6 Ahishari alikuwa mkuu wa nyumba. Adoniramu mwana wa Abda alikuwa mkuu wa watenda kazi.

1
04/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Sulemani alikuwa na maakida kumi na wawili juu ya Israeli yote, ambao walitoa chakula kwa mfalme na watu wake wote. Kila mtu alikuwa na zamu ya kuhudumia kwa mwezi mmoja katka mwaka. \v 8 Majina yao yalikuwa ndiyo haya: Beni Huri, Kutoka milima ya Efraimu; \v 9 Beni Dekeri wa Makazi, Shaalibimu, Bethi Shemeshi, na Elonbethi Hanaan; \v 10 Beni Hesed, wa Arubothi (kutoka kwake alipatikana Sokohi na nchi yote ya Hefa);

1
04/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Ben Abinadabu, wa wilaya yote ya Dori (alikuwa na Tafathi binti wa mfalme ambaye alikuwa mke wake); \v 12 Baana mwana wa Ahiludi, wa Taanaki na Megido, na Beth Shani iliyo upande mwingine wa Zarethani chini ya Yezreel, Kutoak Bethi Shani mpaka Abeli Mehola iliyo upande mwingine wa Jokimeamu; \v 13 Ben Geberi, ya Ramothi Gileadi (kutoka kwake tunapata miji ya Yairi mwana wa Manase, ambayo iko Gileadi, na mkoa wa Arigobu ulikuwa wake, ambao uko Bashani, miji sitini yenye maboma na yenye nguzo za malango ya shaba); \v 14 Ahinadabu mwana wa Ido, wa Mahanaimu;

1
04/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Ahimaazi, wa Naftali (ambaye pia alimwoa Basimathi binti wa Sulemani kuwa mke wake); \v 16 Baana mwana wa Hushai, ya Asherina Bealothi; \v 17 Yehoshafati mwana wa Paruha, kwa Isakari;

1
04/18.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 18 Shimei mwana wa Ela, wa Benjamini; \v 19 na Geberi mwana wa Uri, katika nchi ya Gileadi, ambayo ni nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na Ogi mfalme wa Bashani, na yeye ndiye akida pekee aliyekuwa katika nchi hiyo.

1
04/20.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 20 Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa baharini. Nao walikuwa wakila na kunywa na kufurahi. \v 21 Suleimani alitawala utawala wote kutoka mtoni hadi kwenye nchi ya Wafilisti na hadi kwenye mpaka wa Misri. Wote walileta kodi na walimtumikia Sulemani katika siku za maisha yake yote. \v 22 Mahitaji ya Sulemani kwa siku moja yalikuwa ni Kori thelathini za unga mzuri na kori unga wa ngano, \v 23 makisai kumi walionona, na fahari ishirini wa malisho, na kondoo mia moja, nje ya ayala, paa, na kulungu na kuku walionona.

1
04/24.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 24 Kwa kuwa utawala wake ulikuwa zaidi ya nchi yote upande huu wa mto, kutoka Tifsa mpaka Gaza, juu ya wafalme wote wa upande huu wa mto, naye alikuwa na amani pande zote. \v 25 Yuda na Israeli waliishi kwa usalama, kila mtu chini y a mzabibu wake na chini ya mtini wake, kutoka Dani mpaka Beerisheba, siku zote za Sulemani.

1
04/26.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 26 Sulemani alikuwa na mabanda ya farasi arobaini elfu kwa ajili ya magari yake, na wapanda farasi elfu kumi na mbili. \v 27 Na maakida walileta chakula kwa Sulemani na kwa wale walioketi kwenye meza ya mfalme Sulemani, kila mtu katika mwezi wake. Walihakikisha hakuna kinachopungua. \v 28 Na pia walileta kwenye eneo husika shayiri na majani kwa ajili ya wale farasi wa magari na kwa wale farasi wa mbio kila mmoja alileta kadri alivyoweza.

1
04/29.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 29 Mungu alimpa Sulemani hekima kubwa, ufahamu, na upana wa uelewa kama mchanga wa baharini. \v 30 Hekima ya Sulemani ilizidi hekima ya watu wote wa mashariki na hekima yote ya Misri. \v 31 Alikuwa na hekima kuliko wanaume wote - kuliko Ethani Muezrahi, Hemani, Kaliko, na Darda, wana wa Maholi - na habari zake zikaenea hadi kwenye mataifa yote yaliyomzunguka.

1
04/32.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 32 Aliongea mithali elfu tatu na idadi ya nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano. \v 33 Aliifafanua mimea, kuanzia mierezi iliyoko Lebanoni hadi Hisopo imeao ukutani. Aliwafafanua wanyama, ndege, vitu vitambaavyo na samaki. Watu walikuja kutoka mataifa yote kuisikia hekima ya Sulemani. \v 34 Watu walikuja kutoka falme zote za duniani waliosikia juu ya hekima yake.

1
05/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Hiramu mfalme wa Tiro aliwatuma watumishi wake kwa Sulemani kwa kuwa alisikia kuwa walikuwa wamemtawaza kuwa mfalme mahali pa baba yake, kwani Hiramu alimpenda Daudi. \v 2 Sulemani akatuma ujumbe kwa Hiramu, akisema, \v 3 "Unajua kuwa Daudi baba yangu hakujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wake kwa sababu ya vile vita vilivyomzunguka, kwa kuwa wakati wa uhai wake BWANA alikuwa akiweka maadui wake chini ya nyayo za miguu yake.

1
05/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 Lakini sasa BWANA amenipa mimi pumziko toka pande zote. Hakuna maadui wala majanga. \v 5 Kwa hiyo ninakusudia kujenga hekalu kwa jina la BWANA, Mungu wangu, kama BWANA alivyosema kwa Daudi baba yangu, akisema, 'Mwanao ambaye nitamweka kwenye kiti chako cha enzi mahali pako, ndiye atakayenijengea hekalu kwa jina langu.'

1
05/06.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 6 Kwa hiyo sasa amuru wakate mierezi kutoka Lebanoni kwa ajili yangu. Watumishi wangu wataungana na watumishi wako, nami nitakulipa kwa ajili ya watumishi wako ili kwamba upate malipo mazuri kwa kila kitu utakchokubali kukifanya. Kwa kuwa unajua kuwa hakuna mtu mioingoni mwetu anayejua kukata miti kama Wasidoni."

1
05/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Hiramu aliposikia maneno ya Sulemani, akafurahi sana akasema, "BWANA na abarikiwe leo, ambaye amempa Daudi mwana wa hekiima juu ya kundi hili kubwa." \v 8 Hiramu akatuma neno kwa Sulemani, akisema, "Nimeupata ujumbe ule ulionitumia. Nitatoa miti yote ya mierezi na miti ya miberoshi ambayo unahitaji.

1
05/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Watumishi wangu wataileta miti kutoka Lebanoni hadi baharini, nami nitaiendesha baharini mpaka mahali utakaponielekeza. Nitaigawa pale, nawe utaichukua. Utafanya kile ninachohitaji kwa kuwapa chakula watumishi wangu."

1
05/10.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 10 Kwa hiyo Hiramu akampa Sulemani miti yote ya mierezi na miti ya miberoshi ambayo alihitaji. \v 11 Sulemani akampa Hiramu kori ishirini elfu za ngano kwa ajili ya chakula cha watumishi wake na kori ishirii za mafuta safi. Sulemani akavitoa hivi kwa Hiramu mwaka baad ya mwaka. \v 12 BWANA akampa Sulemani hekima, kama alivyokuwa amemwahidi. Kulikuwa na amani kati ya Hiramu na Sulemani na wote wawili wakafanya agano.

1
05/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Mfalme Sulemani akaandaa wafanya kazi kutoka Israeli yote. Idadi ya watenda kazi walioandaliwa ilikuwa wanaume elfu thelathini. \v 14 Aliwatuma kwenda Lebanoni, aliwatuma kwa zamu ya watu elfu kumi kila mwezi. Kwa mwezi mmoja walienda Lebanoni na miezi miwili walikaa nyumbani. Adoniramu ndiye aliyekuwa msimamizi wa watenda kazi.

1
05/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Sulemani alikuwa na watu elfu sabini waliokuwa wabeba mizigo na watu elfu themanini wa kukata mawe milimani, \v 16 zaidi ya hao, walikuwepo maakida 3, 300 ambao pia waliokuwa wakiisimamia hiyo kazi.

1
05/17.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 17 Kwa amri ya mfalme walileta mawe makubwa ya thamani kwa ajili ya kulaza kwenye msingi wa hekalu. \v 18 Kwa hiyo wajenzi wa Sulemani na wajenzi wa Hiramu na Wagebaliti walifanya kazi ya kukata na kuandaa mbao kwa ajili ya ujenzi wa hekalu.

1
06/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Kwa hiyo Sulemani akaanza kulijenga hekalu. Hii ilikuwa mwaka wa 480 baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Sulemani huko Israeli, katika mwezi wa Ziv, ambao ndio mwezi wa pili. \v 2 Hekalu ambalo mfalme Sulemani alimjengea BWANA lilikuwa na urefu wa mita 27, na upana wa mita 9, na kimo cha mita 13. 5.

1
06/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Na ukumbi uliokuwa mbele ya hekalu ulikuwa na urefu wa mita 9 na upana wa mita 4. 5 sawa na upana wa sehemu kuu ya hekalu. \v 4 Lile hekalu alilitengenezea madirisha ambayo fremu zake kwa nje yalifanya yaonekane membamba kuliko ile sehemu ya ndani.

1
06/05.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 5 Na ukuta wa nyumba aliuzungushia vyumba kuzunguka pande zake, kushikamana na vyumba vya nje na vya ndani ya hekalu. Akajenga vyumba katika pande zote. \v 6 Kile chumba cha chini kilikuwa na upana wa mita 2. 3, kile cha kati kilikuwa na upana wa mita 2. 8. na kile cha tatu kilikuwa na upana wa mita 3. 2. upande wa nje akaupunguza ukuta wa nyumba pande zote, ili boriti zisishikamane ukutani mwa nyumba.

1
06/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Hekalu lilijengwa kwa mawe yaliyokuwa yamechongwa chimboni. Hakuna nyundo, wala shoka au chombo chochote cha chuma kilisikika wakati hekalu lilipokuwa likjengwa. \v 8 Upande wa kusini wa hekalu kulikuwa na lango la chini, ambalo mtu hupanda kwa madaraja mpaka juu kwenye chumba cha kati, na kutoka chumba cha kati hadi chumba cha tatu.

1
06/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Kwa hiyo Sulemani akalijenga hekalu mpaka akalimaliza, akalifunika hekalu kwa boriti na mbao za mwerezi. \v 10 Akajenga vyumba vya pembeni mwa hekalu, kila upande mita 2. 3 kwenda juu. Navyo vikaunganishwa na hekalu kwa mbao za mierezi.

1
06/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Neno la BWANA likamjia Sulemani, likisema, \v 12 "Kuhusu hili hekalu ambalo unajenga, kama utatatembea katika maagizo yangu na kuhukumu kwa haki, na kutunza amri zangu na kuishi kwa hizo, ndipo ntakapozithibitisha ahadi zangu na wewe ambazo niliziahidi kwa baba yako Daudi. \v 13 Nitaishi kati ya watu wa Israeli nami sitawatupa."

1
06/14.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 14 Kwa hiyo Sulemani akalijenga hekalu mpaka akalimaliza. \v 15 Kisha akajenga kuta za ndani za hekalu kwa mbao za mwerezi. Kuanzia sakafu ya hekalu hadi boriti za juu, kwa ndani akazifunika kwa miti, na akaifunika sakafu kwa mbao za miberoshi.

1
06/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Alijenga mita 9 ndani ya hekalu kwa mbao za miberoshi kutoka sakafuni hadi juu. Hiki ni chumba cha ndani, cha patakatifu sana. \v 17 Ule ukumbu mkuu, ulikuwa mahali pakatifu amabao ulikuwa mbele ya patakatifu sana, ulikuwa wa mita 18. hapo kulikwa na mbao za mwerezi ndani ya hekalu, zilizokuwa zimechongwa kwa sura ya vibuyu na maua yaliyochanua. \v 18 Zote zilikuwa za mierezi kwa ndani. Hapakuonekana chochote ndani kilichokuwa kimetengenezwa kwa mawe.

1
06/19.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 19 Sulemani alitengeneza kile chumba cha ndani kwa lengo la kuweka sanduku la agano la BWANA. \v 20 Kile chumba cha ndani kilikuwa na upana wa mita 9, na kimo cha mita 9. Sulemani alizifunika kuta kwa dhabahu na madhabahu aliifunika kwa mbao za mierezi.

1
06/21.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 21 Sulemani alifunika ndani ya hekalu kwa dhahabu safi na akaweka mikufu ya dhahabu iliyopita mbele ya chumba cha ndani, na kulifunika eneo la mbele kwa dhabahu. \v 22 Akalisakafia kwa dhahabu eneo lote la ndani mpaka akamaliza hekalu lote. Pia akalisakafia kwa dhahabu madhahabu yote ya chumba cha ndani.

1
06/23.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 23 Sulemani akatengeneza makerubi mawili kwa mbao za mizeituni, kila moja lilikuwa na kimo cha mita 4. 5 kwa ajili ya chumba cha ndani. \v 24 Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa mita 2. 3. Kwa hiyo kutoka ncha ya bawa moja hadi ncha ya bawa lingine kulikuwa na umbali wa mita 4. 5. Yule \v 25 kerubi mwingine naye alikuwa na bawa lenye kipimo cha mita 4. 5 Makerubi hawa walikuwa wanafanana kwa umbo na kwa vipimo. \v 26 Kimo cha kerubi mmoja kilikuwa mita 4. 5 na yule wa pili alikuwa hivyo hivyo.

1
06/27.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 27 Sulemani aliwaweka hao kerubi kwenye chumba cha patakatifu sana. Bawa moja la kerubi lilikuwa limeenea kiasi kwamba bawa moja liligusa ukuta huu na bawa la yule wa pili nalo liligusa ukuta wa upande mwingine. Hayo mabawa yalikuwa yanakutana katikati ya chumba cha patakatifu sana. \v 28 Sulemani aliwafunika hao kerubi kwa dhahabu.

1
06/29.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 29 Akazinakshi kuta zote kwa sura za makerubi, miti ya mitende, na maua yaliyochanua, kwa vyumba vya nje na vya ndani. \v 30 Sulemani akalisakafia hekalu kwa dhahabu, kwa vyumba vyote vya ndani na vya nje.

1
06/31.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 31 Sulemani akatengeneza milango ya mbao za mizeituni kwenye lango la kuingia ndani. Aliweka vizingiti na miimo kwenye pande tano. \v 32 Kwa hiyo akatengeneza na milango miwili ya mizeituni, na akainakshi kwa makerubi, na mitende, na maua yaliyochanua. Akasakafia kwa dhahabu na akatandaza dhahabu kwenye makerubi na kwenye mitende.

1
06/33.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 33 Kwa njia hii, akalitengenezea hekalu miimo miwili ya mbao za mizeituni yenye pande nne \v 34 na milango miwili ya mbao za mierezi. Zile mbao mbili za mlango mmoja zilikuwa zikijikunja na mbao mbili za mlango wa pili nazo zilikuwa zikijikunja pia. \v 35 Akazinakshi kwa makerubi, mitende, na maua yaliyochanua, na pia akazisakafia kwa dhahabu juu ya zile nakshi.

1
06/36.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 36 Akalijengs Korido la ndani kwa safu tatu za mawe ya kuchongwa na safu moja ya mhimili wa mierezi.

1
06/37.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 37 Msingi wa hekalu ulijengwa katika mwaka wa nne, wa mwezi wa Ziv. \v 38 Mwaka wa kumi na moja mwezi wa Buli, ambao ndio mwezi wa nane, sehemu zote za hekalu zilimalizika na sharti zake zote. Sulemani alilijenga hekalu kwa miaka saba.

1
07/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Ilimchukua Sulemani miaka kumi na tatu kujenga ikulu yake. \v 2 Aliijenga ikulu iliyoitwa mwitu wa Lebanoni. Urefu wake ulikuwa mita 46, na upanawake ulikuwa mita 23, na kimo chake kilikuwa mita 14. Nayo ilikuwa na safu nne ya nguzo za mierezi na mithili ya mwerezi juu ya nguzo.

1
07/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Paa la ikulu lilikuwa la mwerezi ambalo lilikaa juu ya mihimili. Mihili hiyo ilikuwa imeshikiliwa na nguzo. Kulikuwa na mihimili arobaini na tano, ambayo ilikuwa katika safu kumi na tano. \v 4 Nayo mihimili ilikuwa safu tatu, na kila dirisha lilikabili dirisha lingine katika madaraja matatu. \v 5 Milango yote na miimo ilitengenezwa kwa mraba, na madirisha yalikuwa yakikabiliana katika madaraja matatu

1
07/06.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 6 Akatengeneza baraza lenye uerfu wa mita 23 na upana wa mita 14. Mbele yake kulikuwa na ukumbi ulioezekwa.

1
07/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Sulemani akajenga baraza yenye kiti cha enzi ambacho alitolea hukumu ya haki. Nayo ilikuwa imeezekwa kwa mwerezi kutoka sakafu moja hadi nyingine.

1
07/08.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 8 Nyumba ya Sulemani ambayo alikusudia kuishi, katika behewa nyingine ndani ya sehemu ya chini ya ikulu, ilitengenezwa kwa kazi hiyo hiyo. Pia alimjengea binti wa Farao nyumba kama hii, ambaye alikuwa mke wake

1
07/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Majengo haya yalipmbwa kwa vitu vya thamaini, mawe ya thamani, yaliyochongwa na kukatwa kwa msimeno kufuata vipimo sahihi na kulainishwa pande zote. Mawe ya namna hii ndiyo yale yaliyotumika kuanzia kwenye msingi hadi juu, pia na nje hadi kwenye baraza. \v 10 Msingi ulijengwa kwa mawe makubwa sana na ya thamani yenye urefu wa mita 3. 7 na mengine mita 4. 8.

1
07/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Kwa juu ilipambwa kwa, mawe ya thamani yaliyochongwa sawa sawa kwa msimeno na kwa mihimili ya mierezi. \v 12 Na behewa kubwa iliyokuwa ikizunguka ikulu ilikuwa na safu tatu za mawe yaliyokatwa na safu moja ya mihimili ya mierezi kama ilivyo kwenye baraza la ndani la hekalu la BWANA na ule ukumbi wa hekalu.

1
07/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Mfalme Sulemani alituma watu kumleta Huramu kutoka Tiro. \v 14 Huramu alikuwa mwana wa mjane wa kabila ya Naftali; baba yake alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba. Huramu alikuwa mwingi wa hekima na ufahamu na stadi za kufanya kazi kubwa za shaba. Aliletwa kwa mfalme ili kufanya kazi zilizohusiana na shaba kwa mfalme.

1
07/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Huramu alizilemba zile nguzo mbili za shaba, kila moja ilikuwa na kimo cha mita 8. 3 na mzingo wa mita 5. 5. \v 16 Akatengeneza taji mbili za shaba za kuwekwa juu ya zile nguzo. Kimo cha kila taji ilikuwa mita 2. 3. \v 17 Kulikuwa na nyavu za kuwa kama kazi ya kusuka, na masongo ya mikufu, kwa ajili ya kuvipamba vile vichwa vya nguzo, nayo yailikuwa saba kwa kila kichwa.

Some files were not shown because too many files have changed in this diff Show More