sw_deu_text_ulb/09/09.txt

1 line
411 B
Plaintext

\v 9 \v 10 Wakati nilipoenda juu ya mlima kupokea mbao za mawe, mbao za agano ambalo Yahweh alifanya nanyi, Nilibaki kwenye mlima kwa siku arobaini na usiku arobaini; Wala sikula mkate wala kunywa maji. Yahweh alinipa mbao mbili za mawe zilizoandikwa kwa kidole chake; juu yake kuliandikwa kila kitu kama tu maneno yeote ambayo Yahweh alitangaza kwenu juu ya mlima toka katikati mwa moto siku hiyo ya kusanyiko.