\v 18 Mtafanya kile kilicho sahihi na kizuri katika macho ya Yahwe, kwamba iwe vizuri kwenu, na kwamba muweze kuingia na kumiliki nchi nzuri ambayo Yahwe aliaapa kwa baba zenu, \v 19 kuwaondoa maadui zenu wote mbele zenu, kama Yahwe alivyosema.