\v 9 Yahwe Mungu wako atakufanikisha katika kazi yote ya mkono wako, katika matunda ya mwili wako, katika matunda ya mifugo yako, na katika matunda ya nchi yako, kwa mafanikio; kwa maana Yahwe atafurahia tena mafanikio yako, kama alivyofurahia kwa baba zako. \v 10 Atafanya hivi iwapo utatii sauti ya Yahwe Mungu wako, ili kuzishika amri zake na kanuni zake zilizoandikwa katika kitabu hiki cha sheria, iwapo utamgeukia Yahwe Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote.