sw_deu_text_ulb/27/01.txt

1 line
494 B
Plaintext
Raw Normal View History

\c 27 \v 1 Musa na wazee wa Israeli waliwaamuru watu na kusema, “Zishikeni amri zote ninazowaamuru leo. \v 2 Katika siku mtakapopita juu ya Yordani kwenye nchi ambayo Yahwe Mungu wako anawapatia, mnapaswa kutengeneza mawe kiasi makubwa na kuyachapa kwa lipu. \v 3 Mnatakiwa kuyaandika juu yake maneno yote ya sheria hii pale mtakapovuka; ili muweze kwenda katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako anawapatia, nchi inayotiririka kwa maziwa na asali, kama Yahwe, Mungu wa mababu zenu, alivyowaahidi.