\v 3 \v 4 Hautakula mkate wa chachu pamoja nayo, siku saba utakula mkate usio na chachu, mkate wa mateso; kwa kuwa mlitoka katika nchi ya Misri kwa haraka. Fanya haya katika siku zako zote za maisha yako ili uweze kukumbuka akilini siku mliotoka nchi ya Misri. Hakuna chachu inapaswa kuonekana miongoni mwenu ndani ya mipaka yenu wakati wa siku saba; wala nyama yoyote mnayotoa dhabihu jioni kwa siku ya kwanza inabaki mpaka asubuhi.