sw_rev_text_ulb/16/04.txt

1 line
446 B
Plaintext

\v 4 Malaika wa tatu akamwaga bakuli lake katika mito na katika chemichemi za maji; zikawa damu. \v 5 Nikasikia malaika wa maji akisema, "Wewe ni mtakatifu uliyepo na uliyekuwako, Mtakatifu - kwa sababu umezileta hukumu hizi. \v 6 Kwa sababu walimwaga damu za waamini na manabii, umewapa wao kunywa damu; ndicho wanachostahili." \v 7 Nikasikia madhabahu ikijibu, "Ndiyo! Bwana Mungu mwenye kutawala juu ya vyote, hukumu zako ni kweli na za haki."