sw_mat_text_reg/26/62.txt

1 line
426 B
Plaintext

\v 62 Kuhani Mkuu alisimama na kumwuliza, "Hauwezi kujibu? Hawa wanakushuhudia nini dhidi yako?" \v 63 Lakini Yesu alikaa kimya. Kuhani Mkuu akamwambia,"Kama Mungu aishivyo, nakuamuru utwambie, kama wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu." \v 64 Yesu akamjibu, "Wewe mwenyewe umesema jambo hilo. Lakini nakuambia, toka sasa na kuendelea utamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kulia wenye Nguvu, na akija katika mawingu ya mbinguni."