sw_gen_text_ulb/34/24.txt

1 line
440 B
Plaintext

\v 24 Watu wote wa mji wakamsikiliza Hamori na Shekemu, mwanaye. Kila mwanamme akatahiriwa. \v 25 Katika siku ya tatu, walipokuwa katika maumivu bado, wawili wa wana wa Yakobo (Simoni na Lawi, kaka zake Dina), wakachukua kila mmoja upanga wake na kuushambulia mji ambao ulikuwa na uhakika wa ulinzi wake, nao wakauwa wanamme wote. \v 26 Wakamwua Hamori na Shekemu kwa makali ya upanga. Wakamchukua Dina kutoka nyumba ya Shekemu na kuondoka.