sw_gen_text_ulb/14/03.txt

1 line
498 B
Plaintext

\v 3 \v 4 \v 5 \v 6 3 Hawa wafalme watano wa mwisho waliungana pamoja katika bonde la Sidim (pia likiitwa bahari ya chumvi). 4 Kwa miaka kumi na mbili walimtumikia Kedorlaoma, lakini katika mwaka wa kumi na tatu waliasi. 5 Kisha katika mwaka wa kumi na nne, Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja nae walikuja na kuwashambulia Warefai katika Ashteroth Karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe Kiriathaimu, 6 na Wahori katika mlima wao wa Seiri, mpaka El Parani iliyo karibu na jangwa.