1 line
540 B
Plaintext
1 line
540 B
Plaintext
\c 19 \v 1 Malaika wawili wakaja Sodoma jioni, wakati ambao Lutu alikuwa amekaa langoni mwa Sodoma. Lutu akawaona, akainuka kuwalaki, na akainama uso wake chini ardhini. \v 2 Akasema, "Tafadhali Bwana zangu, nawasihi mgeuke mwende kwenye nyumba ya mtumishi wenu, mlale pale usiku na muoshe miguu yenu. Kisha muamke asubuhi na mapema muondoke." Nao wakasema, "Hapana, usiku tutalala mjini." \v 3 Lakini akawasihi sana, mwishowe wakaondoka pamoja naye, na wakaingia katika nyumba yake. Akaandaa chakula na kuoka mkate usiotiwa chachu, wakala. |