sw_gen_text_ulb/04/13.txt

1 line
475 B
Plaintext

\v 13 Kaini akamwambia Yahwe, "Adhabu yangu ni kubwa kuliko uwezo wangu wa kustahimili. \v 14 Kwa hakika umenifukuza siku hii ya leo kutoka kwenye ardhi hii, na sitaonekana mbele ya uso wako. Nitakuwa mkimbizi na mtu nisiye na makao katika dunia, na yeyote atakaye niona ataniua." \v 15 Yahwe akamwambia, "ikiwa mtu yeyote atamuua Kaini, kisasi kitakuwa juu yake mara saba." Kisha Yahwe akaweka alama juu ya Kaini, ili kwamba kama mtu yeyote akimuona, mtu huyo asimshambulie.