sw_gen_text_ulb/39/07.txt

1 line
482 B
Plaintext

\v 7 \v 8 \v 9 7 Ikawa baada ya hayo mke wa bwana wake akamtamani Yusufu. Akamwambia, "Lala nami." 8 Lakini yeye alikataa na kumwambia mke wa bwana wake, "Tazama, bwana wangu haangalii chochote nikifanyacho nyumbani, na ameweka kila kitu anachokimiliki chini ya uangalizi wangu. 9 Hakuna mtu aliye mkuu katika nyumba hii kuliko mimi. Hajanizuilia chochote isipokuwa wewe, kwa sababu wewe ni mkewe. Ni kwa namna gani basi naweza kufanya uovu mkuu namna hii na kumtenda dhambi Mungu?