Tue Apr 18 2023 13:18:20 GMT-0700 (Pacific Daylight Time)

This commit is contained in:
tsDesktop 2023-04-18 13:18:22 -07:00
parent c4ba7aba13
commit 0464e6a057
6 changed files with 6 additions and 0 deletions

1
29/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\c 29 \v 1 \v 2 \v 3 1 Kisha Yakobo akaendelea na safari yake na akafika katika nchi ya watu wa mashariki. 2 Hata alipotazama, akaona kisima kondeni, na, tazama, makundi matatu ya kondoo yalikuwa yamelala kando yake. Kwani kutoka katika hicho wangeyanywesha makundi, na jiwe juu ya mdomo wa kisima lilikuwa kubwa. 3 Wakati makundi yote yangekusanyika pale, wachungaji wangevingirisha jiwe kutoka katika mdomo wa kisima na kuwanywesha kondoo, na kisha kurudisha jiwe juu ya mdomo wa kisima, mahali pake.

1
29/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 \v 5 \v 6 4 Yakobo akawambia, "Ndugu zangu, ninyi mnatokea wapi?" nao wakasema, "Tunatoka Harani." 5 Akawambia, "Mnamfahamu Labani mwana wa Nahori?" Wakasema, "Tunamfahamu." 6 Akawambia, "Je hajambo?" Wakasema, "Hajambo, na, tazama pale, Raheli binti yake anakuja na kondoo."

1
29/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 \v 8 7 Yakobo akasema, "Tazama, ni mchana. Siyo wakati wa kukusanya kondoo pamoja. Mnapaswa kuwanywesha kondoo na kisha mkaenda na kuwaacha wachunge." 8 Wakamwambia, "Hatuwezi kuwanywesha mpaka makundi yote yakusanyike pamoja. Ndipo wanaume watakapovingirisha jiwe kutoka mlangoni mwa kisima, na ndipo tutakapowanywesha kondoo."

1
29/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 \v 10 9 Wakati bado Yakobo anaongea nao, Raheli akaja pamoja na kondoo wa babaye, kwani alikuwa akiwachunga. 10 Yakobo alipomwona Raheli, binti wa Labani, kaka wa mamaye, na kondoo wa Labani, kaka wa mama yake, Yakobo akaja juu, akalivingirisha jiwe kutoka mlangoni mwa kisima, na akawanywesha kondoo wa Labani, kaka wa mama yake.

1
29/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 \v 12 11 Yakobo akambusu Raheli na akalia kwa sauti. 12 Yakobo akamwambia Raheli kwamba alikuwa ni ndugu wa baba yake, na kwamba alikuwa mwana wa Rebeka. Kisha yeye akakimbia kumwambia baba yake.

1
29/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 \v 14 13 Labani aliposikia habari kuhusu Yakobo mwana wa dada yake, akaenda kukutana naye, akamkumbatia, akambusu, na kumleta nyumbani kwake. Yakobo akamwambia Labani mambo haya yote. 14 Labani akamwambia, "Kwa hakika wewe ni mfupa wangu na nyama yangu." Kisha Yakobo akakaa naye kama mwezi mmoja.