sw_gen_text_ulb/43/21.txt

3 lines
525 B
Plaintext
Raw Normal View History

\v 21 \v 22 \v 23 21 Ikawa, tulipofika katika eneo la kupumzikia, tukafungua magunia yetu, na, tazama, pesa ya kila mtu ilikuwa katika gunia lake, pesa yetu kwa kiasi kamili. Tumeileta katika mikono yetu. 22 Tumekuja na pesa nyingine pia mikononi mwetu ili kununua chakula. Hatujui aliyeziweka pesa katika magunia yetu." 23 Mtunzaji wa nyumba akasema, "Amani iwe kwenu, msiogope.
Mungu wenu na Mungu wa baba yenu ndiye aliyeweka pesa katika magunia yenu. Nilipokea
pesa yenu." Kisha mtunzaji wa nyumba akamleta Simoni kwao.