sw_dan_text_ulb/08/24.txt

1 line
439 B
Plaintext

\v 24 Nguvu zake zitakuwa kubwa, lakini si kwa nguvu zake mwenyewe. Atakuwa wa kustaajabisha kwa kile atakachokuwa anakiharibu; atafanya na kufanikiwa. Atawaangamiza watu wenye nguvu, watu miongoni wa watakatifu. \v 25 Ataufanya udanganyifu usitawi chini ya mkono wake kwa sababu ya ujanja wake. Atawaangamiza watu wengi bila kutegemea. Atainuka pia hata kinyume cha Mfalme wa wafalme, na atavunjwa, lakini si kwa mkono wowote wa binadamu.