sw_dan_text_ulb/08/03.txt

1 line
517 B
Plaintext

\v 3 Nilitazama juu na nikaona mbele yangu kondoo dume lenye mapembe mawili, limesimama pembeni mwa mfereji. Pembe moja lilikuwa refu kuliko jingine, lakini pembe ndefu ilikuwa inakua pole pole kuliko ile fupi na pembe fupi ilirefuka na kuizidi nyingine. \v 4 Niliona kondoo mme akiishambulia magharibi, kisha kaskazini, na baadaye kusini; hakuna mnyama mwingine aliyeweza kusimama mbele yake. Hakuna yeyote aliyeweza kumwokoa yeyote katika mkono wake. Alifanya chochote kile alichokitaka, na alikuwa mtu mkubwa sana.