sw_dan_text_ulb/07/23.txt

1 line
422 B
Plaintext

\v 23 Hiki ndicho mtu yule alichokisema, 'Kwa habari ya mnyama wanne, utakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia ambao utakuwa tofauti na falme zingine zote. Utaimeza dunia yote, na utaikanyaga yote chini na kuivunjavunja vipande vipande. \v 24 Na kuhusu pembe kumi, kutoka katika ufalme huu, wafalme kumi watainuka, na mwingine atainuka baada yao. Atakuwa wa tofauti na wale waliomtangulia, na atawashinda wale wafalme watatu.