sw_dan_text_ulb/07/01.txt

1 line
442 B
Plaintext

\c 7 \v 1 Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza mfalme wa Babelli, Danieli alikuwa na ndoto na maono katika akili zake wakati alipokuwa amelala kitandani kwake. Kisha akayaandika yale aliyoyaona katika ndoto. Aliandika matukio ya muhimu sana: \v 2 Danieli alieleza, "Usiku katika ndoto zangu niliona pepo nne za mbinguni zilikuwa zinaitikisa bahari kuu. \v 3 Wanyama wakubwa wanne, kila mmoja alikuwa tofauti na mwenzake, walitoka katika bahari.