sw_dan_text_ulb/06/04.txt

1 line
438 B
Plaintext

\v 4 Basi watawala wakuu wengine na magavana wa majimbo walitafuta makosa katika kazi ambazo Danieli alizifanya kwa ufalme, lakini hawakuweza kuona ufisadi au kushindwa katika majukumu yake kwa sababu alikuwa mwaminifu. Hakuna kosa au uzembe uliopatikana ndani yake. \v 5 Kisha watu hawa wakasema, "Hatukuweza kupata sababu yoyote ya kumshitaki huyu Danieli isipokuwa tukitafuta kitu fulani dhidi yake kuhusiana na sheria za Mungu wake.'"