sw_dan_text_ulb/03/16.txt

1 line
420 B
Plaintext

\v 16 Shadraka, Meshaki, na Abednego wakamjibu mfalme, "Nebukadneza, hatuhitaji kukujibu wewe katika jambo hili. \v 17 Kama kuna jibu, ni kwamba Mungu wetu ambaye tunamtumikia anaweza kutuhifadhi sisi salama katika tanuru la moto, na atatuokoa sisi katika mkono wako, mfalme. \v 18 Kama sivyo, na ijulikane kwako, wewe mfalme, kwamba hatutaiabudu miungu yako, na wala hatutaisujudia wenyewe sanamu ya dhahabu uliyoiweka.