sw_dan_text_ulb/02/14.txt

1 line
446 B
Plaintext

\v 14 Ndipo Daniel alipomjibu kwa busara na umakini, Arioki, kamanda wa walinzi wa mfalme, ambaye alikuwa amekuja kuwaua wale wote waliojulikana kuwa na hekima katika Babeli. \v 15 Danieli alimwuliza kamanda wa mfalme, " Kwanini amri ya mfalme ni ya haraka hivyo?" Hivyo, Arioki akamwambia Danieli kile kilichotokea. \v 16 Ndipo Danieli aliingia ndani na akaomba ahadi ya muda wa kuonana na mfalme ili kwamba aweze kuwasilisha tafsiri kwa mfalme.