sw_dan_text_ulb/02/07.txt

1 line
517 B
Plaintext

\v 7 Wakamjibu tena na kusema, "Mfalme na atuambie, watumishi wake, ndoto nasi tukwambia maana yake." \v 8 Mfalme akawajibu, " Ninajua kwa hakika mnahitaji muda zaidi kwa sababu mmeona maamuzi yangu ni magumu kuhusu jambo hili. \v 9 Lakini kama hamtaweza kuniambia ndoto, kuna sentensi moja tu kwa ajili yenu. Mmeamua kuandaa uongo na maneno ya kudanganya ambayo mmekubaliana kwa pamoja kuniambia mpaka pale nitakapobadili akili zangu. Basi, niambieni ndoto, na kisha nitajua kuwa mnaweza kuitafsiri kwa ajili yangu."