\v 10 Mto wa moto ulitiririka kutoka mbele yake, na maelfu elfu ya watu walimtumikia, na wengine elfu kumi mara elfu walikuwa wamesimama mbele yake. Na mahakama iliitishwa, na vitabu vilifunguliwa.