\v 17 Katika mwaka wa thelathini na tisa wa Ahazia mfalme wa Yuda, Menahemu mwana wa Gadi akaanza kutawala; alitawala kwa miaka kumi katika Samaria. \v 18 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa BWANA. Katika maisha yake yote, hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye alifanya Israeli kufanya dhambi.