sw_1ki_text_ulb/13/14.txt

1 line
561 B
Plaintext

\v 14 \v 15 \v 16 \v 17 14 Yule nabii mzee akamfuata yule mtu wa Mungu na akamkuta amekaa chini ya mti wa mwaloni; akamwambia, "Je, wewe ndiye mtu wa Mungu aliyetoka Yuda?" Naye akamjibu, "Mimi ndiye." 15 Kisha yule nabii mzee akamwambia, "twende nyumbani kwangu ukale chakula." 16 Yule mtu wa Mungu akamjibu, "Siwezi kurudi na wewe wala kuingia ndani na wewe, tena sitakula chakula wala kunywa maji pamoja na wewe mahali hapa, 17 kwa sababu niliamuriwa hivyo kwa neno la BWANA, 'Hautakula chakula wala kunywa maji kule, wala kurudi kwa njia utakayokuja nayo.'"