sw_1ki_text_ulb/13/01.txt

1 line
636 B
Plaintext

\c 13 \v 1 \v 2 \v 3 1 Mtu wa Mungu alikuja tokea Yuda kwa neno la BWANA kule Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa amesimama karibu na madhabahu ili kufukiza uvumba. 2 Akalia kinyume na zile madhabahu kwa neno la BWANA: "Ee madhabahu, madhabahu" hivi ndivyo asemavyo BWANA, 'Tazama, mwana aitwaye Yosia atazaliwa katika familia ya Daudi, na juu yenu atawachinja makuhani ambao sasa wanafukiza uvumba mahali hapa pa juu kwa ajili yako. Juu yako watachoma mifupa ya watu.'" 3 Kisha mtu wa Mungu akatoa ishara siku hiyohiyo, akisema, "Hii ndiyo ishara ya kwamba BWANA amesema: 'Tazama, madhabahu zitavunjika, na majivu yaliyo juu yatamwagika."