swc_mat_text_reg/02/16.txt

1 line
306 B
Plaintext

\v 16 Herode alipoona kwamba wale watu wenye elimu wamemudanganya, akakasirika sana. Akatuma watu Betelehemu na popote kandokando yake kwa kuua watoto wote waliokuwa na umri wa miaka miwili na chini yake. Alifanya vile kufuatana na jinsi alivyohakikishwa na wale wenye elimu juu ya wakati nyota ilipotokea.