# Sentensi unganishi Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake. # Tazama, je kufanikwa kwao hakupo mikono mwao mwenyewe? hapa "mikono" inamaanisha nguvu zao au utawala wao. Ayubu anatumia swali hili kutoa changamoto kwa rafiki zake. KT: "Tazama, watu hawa waovu wanasema kwamba wamesababisha mafaniki wao wenyewe!" # Je ni mara ngapi... msiba wao huwajilia? Ayubu anatumia swali hili kusisitiza kuwa yeye anaona kwamba Mungu hawaadhibu waovu mara nyingi. KT: "si mara nyingi ... msiba wao huwapata " # taa ya watu waovu imezimwa Ayubu analinganisha kuzima taa na kufa. KTN: "Mungu husababisha wafe ghafla" # Ni mara ngapi hutokea... katika hasira yake? Ayubu anatumia swali hili la pili kuweka mkazo kuwa inaonekana mara nyingi Mungu huwa hawaadhibu waovu. KTN: "Si mara nyingi ... katika hasira yake." # Ni mara ngapi ... dhoruba huwabeba? Ayubu anatumia swali hili la tatu kuweka mkazo kuwa inaonekana mara nyingi Mungu huwa hawaadhibu waovu.KTN: "Si mara nyingi ... dhoruba huwabeba." # wanakuwa kama mabua mbele ya upepo au kama makapi ambayo huchukuliwa na dhoruba Kifo cha waovu kinaongelewa kana kwamba ni makapi yasiyofaa na mabua yapeperushwayo.KTN: "Mungu huwaondoa kama upepo upeperushao makapi"