# waliasi dhidi ya neno la Mungu ... kukataa maagazi ya Aliye juu. Misemo hii ina maana sawa na inasisitiza jinsi walivyomuasi Mungu, ambayo ndio sababu ya kufungwa. # Alinyenyekesha mioyo yao kupitia ugumu Hapa moyo unamaanisha mtu, lakini mahususi mapenzi yake. "Aliwanyenyekesha kwa kuwaruhusu wapitie magumu" # ugumu Maana zinazowezekana ni 1) "tabu" au 2) "kazi ngumu" # walijikwaa na hakuwepo mtu kuwasaidia kuinuka Neno "kujikwaa" linamaanisha wakati watu hawa walijikuta kwenye nyakati ngumu sana. "waliingia taabuni na hakuwepo mtu wakuwakomboa" # Kisha wakamuita Yahwe katika tabu yao Inaashiriwa kuwa wanaomba kwa Yahwe ili awasaidie. "Kisha wakaomba kwa Yahwe kuwasaidia katika shida yao" # dhiki yao "taabu" au "mateso" # akawatoa Hapa Daudi anaelezea Yahwe kuwaokoa kutoka dhiki yao kana kwamba dhiki ilikuwa sehemu ya kimwili ambayo alikuwa akiwatoa.