# usiwaache wafurahi juu yangu "usiwaache wafurahi kwa sababu ninateseka" # waseme moyoni mwao Hii ni lahaja inayomaanisha kujisemesha. "wajisemeshe" # Aha Huu ni mshangao unaotumika wakati kitu kinaonekana ghafla au kueleweka. Unaweka mkazo katika kauli inayofuata. "Ndio" # tumepata tunalichokuwa tunataka Inadokezwa kuwa adui wa mwandishi walitaka atangazwe kuwa na hatia. "ametangazwa kuwa na hatia kama tulivyokuwa tunatamani!" # Tumemmeza Adui wa mwandishi wanazungumzia uharibifu wake kana kwamba waoni wanyama pori waliommeza. "Tumemwangamiza" # shangaze "aibishe" au "fadhaishe" # Na wale wanao nidhihaki wafunikwe na aibu na kukosa heshima Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Na uwafunike kwa aibu na kukosa heshima wale wanao nidhihaki" # nidhihaki kumtukana mtu ili kumkasirisha # wafunikwe na aibu na kukosa heshima Hapa aibu na kukosa heshima zinazungumziwa kana kwamba zilikuwa nguo za aibu ambazo mwandishi aliweza kuvaa. Nomini dhahania hizi zinaweza kuelezwa kama vitenzi. "waaibishwe na kukosa heshima" # aibu na kukosa heshima Haya maneno yana maana za kukaribiana na yanatumika kuonesha ni kiasa gani watashushwa.