Add 'heb/front/Intro.md'

This commit is contained in:
Rick 2021-05-28 20:07:10 +00:00
parent 0b02c62f3e
commit d5c2ef7c84
1 changed files with 61 additions and 0 deletions

61
heb/front/Intro.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,61 @@
# Utangulizi wa Waebrania
## Sehemu ya 1: Utangulizi wa jumla
### Muhtasari wa kitabu cha Waebrania
1. Yesu ni mkuu kuliko manabii wa Mungu na malaika (1:1-4:13)
1. Yesu ni mkuu kuliko makuhani wanaohudumu katika hekalu la Yerusalemu (4:14-7:28)
1. Huduma ya Yesu ni kuu kuliko agano la kale Mungu alilofanya na watu wake (8:1-10:39)
1. "Imani ni kama nini (11:1-40)
1. Kutia moyo kuwa mwaminifu kwa Mungu (12:1-29)
1. Mahimizo ya kumalizia na salamu (13:1-25)
### Nani aliandika kitabu cha Waebrania?
Hakuna ajuaye mwandishi wa Waebrania. Wasomi wanapendekeza watu kadhaa ambao kuna uwezekano waliandika Waebrania. Watu hawa ni Paulo, Luka na Barnaba. Tarehe ya kukiandika pia hakijulikani. Wasomi wengi wanafikiri kiliandikwa miaka mbele ya mwaka wa 70 A.D..Yerusalemu iliharibiwa 70 A.D. lakini mwandishi wa kitabu hiki anazungumzia Yerusalemu kana kwamba ulikuwa bado haujaharibiwa.
### Kitabu cha Waebrania kinahusu nini?
Katika kitabu cha Waebrania, mwandishi anaonyesha kwamba Yesu alitimiza unabii za Agano la Kale. Mwandishi alifanya hivi kuwahimiza Wakristo Wayahudi kwamba Kristu ni bora kuliko kitu chochote Agano la Kale lingepeana.Yesu ndiye Kuhani Mkuu bora. Yesu pia ndiye dhabihu bora. Dhabihu ya wanyama yalikosa maana kwa sababu dhabihu ya Yesu ilitolewa mara moja na ya mwisho. Kwa hivyo Yesu ndiye njia pekee ya watu kukubalika na Mungu.
### Kichwa cha kitabu hiki kinastahili kutafsiriwa namna gani?
Watafsiri wanaweza kuamua kukiita kitabu hiki kutumia kichwa chake cha kitamaduni ,"Waebrania" ama wanaweza kuchagua kichwa kinachoeleweka zaidi kama "Barua kwa Waebrania" ama "Barua kwa Wakristo Wayahudi." (Tazama:rc://en/ta/man/translate/translate-names)
## Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni
### Je, wasomaji wanaweza elewa kitabu hiki bila kufahamu kuhusu dhabihu na kazi ya makuhani katika Agano la Kale?
Itakuwa vigumu kwa wasomaji kuelewa kitabu hiki bila kuyaelewa maswala haya. Watafsiri wanaweza pendekeza kuzifafanua baadhi ya dhana hizi za Agano la Kale kwa maelezo ama katika utangulizi wa kitabu hiki.
### Swala la damu limetumika vipi katika kitabu cha Waebrania?
Kuanzia Waebrania 9:7 swala la damu linatumika kuashiria kifo cha mnyama yeyote ambaye alitambikwa kulingana na agano la Mungu pamoja na Israeli. Mwandishi pia anatumia damu kuashiria kifo cha Yesu Kristo.Yesu alikuwa sadaka kamilifu ili Mungu awasamehe watu sababu walimtendea dhambi.(Tazama: rc:/en/ta/man/translate/figs-metonymy)
Kuanzia Waebrania 9:19, mwandishi anatumia swala la kunyunyuzia damu kama tendo la maana ya mfano. Katika Agano la Kale makuhani walinyunyuzia damu ya wanyama waliotolewa sadaka. Hii ilikuwa ni ishara ya faida za kifo cha mnyama kuelekezewa watu ama kitu. Hii ilimaanisha kwamba watu ama kitu kilikubalika/walikubalika kwa Mungu.(Tazama: rc://en/ta/man/translate/translate-symaction)
## Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya tafsiri.
### Maswala ya "Takatifu" na "takaza/takatatifuzwa" yameasilishwa namna gani katika Waebrania kwa ULB?
Maandiko yanatumia maneno kama haya kuashiria maswala mbalimbali.Kwa sababu hiyo, mara nyingi ni vigumu kwa watafsiri kuyawakilisha vyema katika matoleo yao.Kuyatafsiri katika Kiingereza, ULB hutumia sheria zifuatavyo:
* Wakati mwingine maana katika aya huashiria utakatifu. Hii ni muhimu kwa kuelewa injili kwa maana ya kwamba Mungu huwatazama Wakristo kama wasio na dhambi kwa sababu wameungana na Kristo.Swala lingine linalolingana na hili ni kwamba Mungu ni mkamilifu na asiye na doa.Swala la tatu ni kwamba Wakristo hujieleza kwa njia isiyo ya kulaumiwa na siyo na mapungufu yoyote.Katika hali hizi,ULB inatuma "Takatifu", "Mungu Mtakatifu" "wale watakatifu," ama "watu watakatifu."
* Wakati mwingine maana inaashiria Wakristo bila kuashiria jukumu fulani linalotekelezwa nao. Katika hali hizi, ULB inatumia "muumini" ama "waumini" (Tazama:10; 13:24)
* Wakati mwingine maana inaashiria kitu kilichowekwa kando kwa ajili ya Mungu pekee. Kwa hali hii, ULB inatumia "Takaza", "Wekwa kando" "kuweka wakfu kwa" ama "hifadhia" (Tazama: 2:11: 9:13; 10:10, 14, 29; 13:12)
UDB itakuwa na usaidizi wakati watafsiri anafikiria jinsi ya kuwakilisha mawazo haya katika matoleo yao wenyewe.
### Ni maswala gani muhimu katika maandishi ya kitabu cha Waebrania?
Katika mistari ifuatayo, matoleo ya kisasa ya Bibilia yanatofautiana na matoleo ya kale. ULB ina masomo ya kisasa na huweka masomo ya zamani kama maelezo ya chini. Kama kuna tafsiri ya Bibilia katika eneo jumla, watafsiri wanafaa kuzingatia kutumia masomo yaliyo kwenye hayo matoleo. Kama si hivyo, watafsiri wanashauriwa kutumia masomo ya kisasa.
* "Ulimvisha taji la utukufu na heshima" (2:7). Matoleo mengine ya kale yanasoma, "Ulimvisha taji la utukufu na heshima na umemtawaza juu ya kazi ya mikono yako."
* "Wale amabao hawakuungana kwa imani na wale waliotii" (4:2)Matoleo mengine ya zamani husoma, "wale ambao walilisikia bila kuliunganisha na imani".
* "Kristo alikuja kama kuhani mkuu ya mambo mazuri yaliyokuja" (9:11).Matoleo mengine husoma, "Kristu alikuja kama kuhani mkuu ya mambo mema yatakayokuja".
* "Kwa hao waliokuwa wafungwa" (10:34). Matoleo mengine yanasoma, "Kwangu nilioko kwenye minyororo yangu".
* "Walipigwa kwa mawe. Walikatwa kwa msumeno vipande viwili. Waliuawa kwa upanga" (11:37). Matoleo mengine ya kale yanasoma, "Walipigwa kwa mawe. Walikatwa kwa msumeno vipande viwili. Walijaribiwa. Waliuwawa kwa upanga".
* "Hata mnyama akiugusa huo mlima, lazima apigwe kwa mawe" (12:20). Matoleo mengine ya zamani yanasoma, "Hata mnyama akiugusa huo mlima, lazima apigwe kwa mawe ama achomwe kwa mkuki."
(See: [[rc://en/ta/man/jit/translate-textvariants]])