Add 'heb/09/Intro.md'

This commit is contained in:
Rick 2021-06-03 00:08:16 +00:00
parent a2bb580ae5
commit b708748d24
1 changed files with 31 additions and 0 deletions

31
heb/09/Intro.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,31 @@
# Waebrania 09: Maelezo kwa jumla
### Muundo na Mpangilio
Sura hii inaonyesha jinsi Yesu ni bora kuliko hekalu na sheria na masharti yake. Sura hii itakuwa ngumu kuelewa iwapo vitabo vitanu vya kwanza vya Agano la Kale havijatafsiriwa.
### Dhana muhimu katika sura hii
#### Agano la urithi
Agano la urithi ni hati ya kisheria ambayo huelezea kile ambacho kitafanyikia mali ya mtu baada ya kifo chake.
#### Damu
Katika Agano la kale, Mungu alikuwa ameamuru Waisraeli kutoa dhabihu ili dhambi zao zisamehewe. Kabla hawajatoa dhabihu hizi, walipaswa kuwaua wanyama na siyo kutoa tu miili ya wanyama hao lakini pia damu zao. Kutoa damu ni tamathali ya kumuua binadamu ama mnyama.Mungu alipeana uhai na damu yake kama dhabihu/kafara alipowaruhusu watu kumuua.Mwandishi wa Waebrania anasema kwamba hii dhabihu ni bora kuliko dhabihu ya agano la kale.(Tazama: rc://en/ta/man/translate/figs-metaphor and rc://en/tw/dict/bible/kt/covenant)
#### Kurudi kwa Kristo
Yesu atarudi kumaliza kazi aliyoianzisha wakati alipokufa ili Mungu angewasamehe watu dhambi zao. Atamalizia kuwaokoa watu wanaomngojea.(Tazama: rc://en/tw/dict/bible/kt/save)
### Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii
#### Agano la Kwanza
Hii inaashiria agano ambalo Mungu alifanya na Musa. Hata hivyo, kabla hajafanya agano hili, Mungu alikuwa amefanya agano na Abrahamu. Lakini hili lilikuwa ni agano la kwanza ambalo Mungu alifanya na watu wa Israeli. Unaweza amua kutafsiri "agano la kwanza" kama "agano la awali."
## Links:
* __[Hebrews 9:1](../../heb/09/01.md)__
__[<<](../08/intro.md) | [>>](../10/intro.md)__