Add 'luk/23/Intro.md'

This commit is contained in:
Rick 2021-05-05 21:53:39 +00:00
parent b47bbf2b40
commit 92d4c4a0b4
1 changed files with 31 additions and 0 deletions

31
luk/23/Intro.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,31 @@
# Luka 23 Maelezo ya Jumla
### Muundo na upangiliaji
ULB huweka mbele kidogo mstari wa mwisho wa sura hii kwa sababu unaunganishwa zaidi na sura ya 24 kuliko sura ya 23.
### Dhana maalum katika sura hii
#### "Walianza kumshtaki"
Watu hawa hawakuwa wakimshtaki Yesu kwa kufanya uovu, bali mashtaka yao yalikuwa ya uwongo. Waligeuza ukweli ili kumfanya Pilato kumhukumu Yesu kufa.
#### "Pazia la hekalu likagawanyika na kuwa vipande viwili"
Hii ni ishara muhimu. Pazia ilikuwa mfano ya utenganisho kati ya Mungu na mwanadamu. Mungu hakuweza kupatikana moja kwa moja kwa sababu ya utakatifu wake. Kifo cha Kristo kilibadilisha hii. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/holy)
#### Desturi ya Mazishi
Ilikuwa ni desturi katika Israeli ya kale kumzika mtu aliyeheshimika katika kaburi na kutumia mwamba mkubwa kuifunga.
### Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii
#### "Sioni kosa lolote katika mtu huyu.""
Baada ya swali moja rahisi, inaonekana kwamba Pilato anamtangaza Yesu kutokuwa na hatia haraka sana. Hii ni kwa sababu Luka hajaweka maelezo mengi ya mazungumzo ya Yesu na Pilato. Habari hii imeandikwa katika Injili nyingine.
## Links:
* __[Luke 23:01 Notes](./01.md)__
__[<<](../22/intro.md) | [>>](../24/intro.md)__