Add 'mat/23/Intro.md'

This commit is contained in:
Rick 2021-05-03 17:03:11 +00:00
parent 56deca719b
commit 673c93c536
1 changed files with 23 additions and 0 deletions

23
mat/23/Intro.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,23 @@
# Mathayo 23 Maelezo ya Jumla
### Dhana maalum katika sura hii
#### Wanafiki
Unafiki wa Wafarisayo ni neno kuu katika sura hii. Yesu anazungumzia kwa kina kuhusu unafiki huu. Wafarisayo waliunda sheria ambayo hakuna mtu angeweza kutii, na kisha wakawashawishi watu kwamba walikuwa na hatia kwa sababu ya kutotii sheria. Pia, sheria za Wafarisayo ziliwapa sababu za kutotii amri za asili za Mungu za Sheria ya Musa.
### Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii
#### Kutusi
Katika tamaduni nyingi, ni makosa kuwaalumu watu. Maneno mengi katika sura hii yaliyowalenga Wafarisayo yanaweza kuchukuliwa kama matusi. Wanaitwa "wanafiki," "viongozi vipofu," "wajinga," na "nyoka." Yesu anatumia maneno haya kuelezea na kuhukumu tabia zao.
#### Kitendawili
Kitendawili ni taarifa inayoonekana kuwa ya ajabu, ambayo ni kana kwamba inajikana yenyewe, lakini kwa hakika sio ya ajabu. Kwa mfano, "aliye mkuu kati yenu atakuwa mtumishi wenu" (Mathayo 23:11-12).
## Links:
* __[Matthew 23:01 Notes](./01.md)__
__[<<](../22/intro.md) | [>>](../24/intro.md)__