Add 'rev/20/Intro.md'

This commit is contained in:
Rick 2021-06-10 20:03:57 +00:00
parent a0d0b357b6
commit 38efbfc77a
1 changed files with 37 additions and 0 deletions

37
rev/20/Intro.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,37 @@
# Ufunuo 20 Maelezo ya jumla
### Muundo na mpangilio
Sura hii inahusu kipindi kinachojulikana kama "ufalme wa kimilenia" kwa sababu ni ufalme wa miaka elfu moja. Sura hii ni muhimu kuelewa matukio ya siku za mwisho na kitabu cha Ufunuo.(Tazama: rc://en/tw/dict/bible/kt/lastday)
### Dhana muhimu katika sura hii
#### Miaka elfu ya utawala wa Kristo
Yesu anaelezewa kama anayetawala kwa miaka elfu moja na nabii zote za maandiko kuhusu amani duniani kote lazima zitatimika. Wasomi wanatofautiana kuhusu iwapo huu ni muda wa ekweli ama ni ishara ya mwanzo wa utawala wa Kristo kwenye mioyo ya watu. Ni vizuri kutafsiri kana kwamba Kristo anatawala kimwili duniani kwa miaka elfu moja na siyo kujaribu kuweka taswira ya kimafumbo katika maandiko. (Tazama: rc://en/tw/dict/bible/kt/prophet)
#### Uasi wa mwisho
Sura hii inafafanua kipindi cha wakati baada ya utawala wa Yesu kinachojulikana kama uasi wa mwisho.Wakati huu,Shetani na watu wengi watajaribu kuasi dhidi ya Yesu. Hii itapelekea ushindi wa mwisho wa Mungu dhidi ya dhambi na uovu kabla ya maisha ya milele kuanza. (Tazama:rc://en/tw/dict/bible/kt/sin]], [[rc://en/tw/dict/bible/kt/evil]] na [[rc://en/tw/dict/bible/kt/eternity)
#### Kiti kikubwa cheupe cha enzi
Hii ni hukumu muhimu mbinguni baada ya uasi wa mwisho.Wakati wa hukumu hii, watu walio na imani kwa Mungu wanatenganishwa na wale wanaomkataa. (Tazama: rc://en/tw/dict/bible/kt/judge]], [[rc://en/tw/dict/bible/kt/heaven]] and [[rc://en/tw/dict/bible/kt/faith)
### Tamathali muhimu za usemi katika sura hii
#### Kitabu cha uzima
Hii ni mfano wa maisha ya milele. Walio na uzima wa milele wanasemekana kuwa na majina yao yameandikwa katika kitabu hiki cha uzima.. (Tazama: rc://en/ta/man/translate/figs-metaphor)
### Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii.
#### Kuzimu na ziwa la moto
Hizi zinaoenakana kuwa mahali mbili tofauti. Mtafsiri anaweza kufanya utafiti zaidi kupata jinsi ya kuzitofautisha hizi mahali mbili lakini zisifananishwe katika tafsiri. (Tazama: rc://en/tw/dict/bible/kt/hell)
## Links:
* __[Revelation 20:01 Notes](./01.md)__
__[<<](../19/intro.md) | [>>](../21/intro.md)__