Add 'tit/front/Intro.md'

This commit is contained in:
Rick 2021-05-28 16:41:52 +00:00
parent 49aeaca897
commit 22b1b02b2f
1 changed files with 37 additions and 0 deletions

37
tit/front/Intro.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,37 @@
# Utangulizi wa Tito
## Utangulizi wa Jumla
### Muhtasari wa kitabu cha Tito
1. Paulo anamshauri Tito kuwateua viongozi wanaomcha Mungu (1:1-16)
1. Paulo anamshauri Tito kuwafundisha watu kuishi maisha ya kumcha Mungu (2:1-3:11)
1. Paulo anamalizia kwa kuelezea baadhi ya mipango yake na kutuma salamu kwa waumini. (3:12-15)
### Nani aliandika kitabu chaTito?
Paulo aliandika Kitabu cha Tito. Hapo awali alijulikana kama Saulo. Alitokea mji wa Tarso. Kabla ya kuwa Mkristo alikuwa Mfarisayo na alikuwa akiwatesa sana Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara nyingi katika himaya nzima ya Warumi akiwahubiria watu kumhusu Yesu
### Kitabu cha Tito kinahusu nini?
Paulo alimwandikia barua hii Tito, mfanyakazi mwenza aliyekuwa anayaongoza makanisa ya Kisiwa cha Krete.Paulo alimwelekeza jinsi ya kuwachagua viongozi wa kanisa.Paulo pia alifafanua jinsi waumini walipaswa kutendeana.Na akawahimiza wote waishi maisha yanayompendeza Mungu.
### Kichwa cha kitabu hiki kinafaa kitafsiriwe vipi?
Watafsiri wanaweza kukiita kitabu hiki kutumia kichwa chake cha kitamaduni, "Tito" ama wanaweza kuchagua kichwa kinachoeleweka zaidi kama, "Barua ya Paulo kwa Tito," ama "Barua kwa Tito." (Tazama: rc://en/ta/man/translate/translate-names)
## Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni
### Watu wanaweza tumikia kanisa katika majukumu gani?
Kuna mafundisho fulani katika kitabu cha Tito kuhusu iwapo mwanamke ama mwanamume waliopeana talaka wanaweza kutumikia katika nafasi za uongozi kwenye kanisa. Wasomi wanatofautiana kuhusu maana ya mafundisho haya.Mafundisho zaidi kuhusu haya mambo yatakuwa ya muhimu kabla ya kukitafsiri kitabu hiki.
## Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya tafsiri
#### Umoja na wingi wa "wewe" na "ninyi"
Katika kitabu hiki, neno "mimi" linaashiria Paulo. Mara nyingi neno "wewe" inaashiria mtu moja, ndiye Tito, isipokuwa katika 3:15. (Tazama:rc://en/ta/man/translate/figs-exclusive and rc://en/ta/man/translate/figs-you)
### Ni nini maana ya "Mungu mkombozi wetu"?
Hili ni tamko la kawaida katika barua hii. Paulo alitaka wasomaji wafikirie jinsi Mungu aliwasamehe kupitia kwa Kristo baada ya hao kumtendea dhambi. Na kwa kuwasamehe aliwaokoa kutoka kuadhibiwa wakati atakapowahukumu watu wote. Tamko sawa na hili katika barua hii ni, "Mungu wetu mkuu na Mkombozi Yesu Kristo."