Add 'mrk/03/Intro.md'

This commit is contained in:
Rick 2021-05-03 18:38:27 +00:00
parent a5b39acfa7
commit 15ab641976
1 changed files with 41 additions and 0 deletions

41
mrk/03/Intro.md Normal file
View File

@ -0,0 +1,41 @@
# Marko 03 Maelezo ya Jumla
### Dhana maalum katika sura hii
#### Sabato
Ilikuwa kinyume cha sheria ya Musa kufanya kazi siku ya sabato. Mafarisayo waliamini kumponya mtu mgonjwa siku ya Sabato ilikuwa "kazi," hivyo wakasema kwamba Yesu alifanya makosa wakati alimponya mtu siku ya Sabato. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/lawofmoses)
#### "Kukufuru dhidi ya Roho"
Hakuna mtu anayejua kwa hakika hatua ambazo watu hufanya au maneno gani wanayosema wanapotenda dhambi hii. Hata hivyo, labda wao humtusi Roho Mtakatifu na kazi yake. Sehemu ya kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwafanya watu kuelewa kuwa wao ni wenye dhambi na wanahitaji kusamehewa na Mungu. Kwa hiyo, yeyote asiyejaribu kuacha dhambi huenda anakufuru Roho. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/blasphemy and rc://en/tw/dict/bible/kt/holyspirit)
### Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii
#### Wanafunzi kumi na wawili
Yafuatayo ni orodha ya wanafunzi kumi na wawili:
Katika Mathayo:
Simoni (Petro), Andrea, Yakobo mwana wa Zebedayo, Yohana mwana wa Zebedayo, Filipo, Bartholomeo, Tomasi, Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Tadayo, Simoni wa Zeloti na Yuda Isikariote.
Katika Marko:
Simoni (Petro), Andrea, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana mwana wa Zebedayo (ambao aliwaita Boanerge, yaani, wana wa ngurumo), Filipo, Bartholomeo, Mathayo, Tomasi, Yakobo mwana wa Alifayo, Tadayo Simoni wa Zeloti na Yuda Isikariote.
Katika Luka:
Simoni (Petro), Andrea, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartholomeo, Mathayo, Tomasi, Yakobo mwana wa Alifayo, Simoni (aitwaye Zeloti), Yuda mwana wa Yakobo, na Yuda Isikariote.
Thadayo labda ni Yuda, mwana wa Yakobo.
#### Ndugu na Dada
Watu wengi huwaita wale ambao wana wazazi sawa "ndugu" na "dada" na kuwafikiria kama watu muhimu zaidi katika maisha yao. Watu wengi pia huita wale walio na babu na nyanya sawa "ndugu" na "dada." Katika sura hii Yesu anasema kwamba watu muhimu zaidi kwake ni wale wanaomtii Mungu. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/brother)
## Links:
* __[Mark 03:01 Notes](./01.md)__
__[<<](../02/intro.md) | [>>](../04/intro.md)__