sw_ulb/57-TIT.usfm

70 lines
5.6 KiB
Plaintext

\id TIT
\ide UTF-8
\h Tito
\toc1 Tito
\toc2 Tito
\toc3 tit
\mt Tito
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo, kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu na maarifa ya kweli iletayo utauwa,
\v 2 Wapo katika tumaini la uzima wa milele ambao Munguasiyeweza kusema uongo, aliuahidi tangu milelekabla ya enzi zote za wakati.
\v 3 Kwa wakati uliofaa alilifunua neno lake katika ujumbe alionipa mimi kuhubirilinipasa kufanya hivi kwa amri ya Mungu mwokozi wetu.
\v 4 Kwa Tito, mwana wa kweli katika imani yetu tunayoshiriki sote. Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba na Yesu Kristo mwokozi wetu.
\v 5 Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili upate kupanga mambo ambayo bado hayajakamilika na kuweka wakfu wazee wa kanisa kwa kila mji kama nilivyokuagiza.
\v 6 Mzee wa kanisa lazima asiwe na lawama, mme wa mke mmoja, aliye na watoto waaminifu wasioshuhundiwa mabaya au wasiotii.
\v 7 Ni muhimu kwa mwangalizi, kama msimamizi wa nyumba ya Mungu, asiwe na lawama. Asiwe mtu mwenye kiburi, hakasiriki haraka, si mraibu wa mvinyo, si mgomvi na asiwe mwenye tamaa.
\v 8 Badala yake: awe mtu mkarimu, apendaye wema, mwenye busara, mnyoofu, mtakatifu na anayejidhibiti.
\v 9 Awezaye kushika sana ujumbe wa kuaminika uliofundishwa, ili aweze kuwatia moyo wengine kwa mafundisho ya ukweli na kuwarekebisha wale wanaompinga.
\p
\v 10 Kwa kuwa kuna waasi wengi, wanenao matupu na wandanganyao, hasa wale wa tohara. Maneno yao ni ya upuuzi. Wanandanganya na kuwaongoza watu katika upotovu.
\v 11 Ni lazima kuwazuiawatu kama haoWanafundisha yale wasiopaswa kwa faida za aibu na kuharibu familia zote.
\v 12 Mmoja wa manabii wao amesema “Wakrete daima ni waongo, wanyama wabaya, walafi wavivu.”
\v 13 Ushuhuda huu ni kweli. Kwa hiyo warekebishe kwa nguvu, ili kwamba waweze kusema kweli katika imani,
\v 14 Wewe usijihusishe na hadithi zisizo za kweli za Kiyahudi au amri za watu, ambao hurudisha nyuma ukweli.
\v 15 Kwa wote walio safi, vitu vyote ni visafi. Bali kwa walioharibika na wasioamini, hakuna kilicho kisafi, lakini akili zao na dhamiri zao zimeharibika.
\v 16 Wanakiri kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Wao ni machukizo, wasiotii, na wasiofaa kitu kwa kazi yo yote njema.
\c 2
\cl Sura 2
\p
\v 1 Lakini wewe, sema yale yanayo ambatana na mafundisho ya kweli.
\v 2 Wafundishe wanaume wazee kuwa na kiasi, wenye heshima, wenye busara na timamu katika imani, katika upendo, na katika uvumilivu.
\v 3 Vvyo hivyo, fundisha wanawake wazee kuwa na tabia ya heshima, si wasingiziaji, na wasiwe watumwa wa divai nyingi lakini wawe walimu wa yale yaliyo mema.
\v 4 Na kufundisha wanawake wadogo kuwapenda waume zao na watoto wao,
\v 5 kuwa na busara, wasafi, watunzaji wazuri wa nyumba zao, na kuwatii waume zao wenyewe, ili neno la Mungu lisisemwe kuwa mabaya.
\v 6 Vivyo hivyo, watie moyo vijana wa kiume wawe na busara.
\v 7 Katika njia zote jionyeshe mwenyewe kama mfano wa matendo mema. Katika mfundisho yako onyesha uadilifu, heshima,
\v 8 na ujumbe wa ukweli usioweza kukosolewa, ili kwamba yeyote wakupingao waaibishwe kwa sababu hawana ubaya wa kusema juu yetu.
\v 9 Watumwa na wawatii mabwana zao katika kila kitu, wawafurahishe na sio kubishana nao,
\v 10 wasiwaibie, bali waonyeshe nia njema yote, ili kwa njia zote wailete sifa mafundisho kumhusu Mungu mwokozi wetu.
\p
\v 11 Kwa kuwa neema ya Mungu imeonekana kwa ajili ya wokovu wa watu wote.
\v 12 Inatufundisha kukataa mambo yasiyo ya kimungu na tamaa za kidunia, na kuishi maisha ya kiasi, uadilifu, na utauwa katika zama hizi,
\v 13 huku tukitazamia kupokea tumaini letu lenye baraka, kuonekana kwa utukufu wa Mungu wetu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo.
\v 14 Yesu alijitoa nafsi kwa ajili yetu ili atukomboe na maasi yote na kujitakasia watu maalum walio na hamu ya kufanya matendo mema.
\p
\v 15 Yaseme mambo haya, watie watu moyo kuyatimiza na utoe marekembisho kwa mamlaka yote. Usikubali mtu yeyote akupuuze.
\c 3
\cl Sura 3
\p
\v 1 Wakumbushe kunyenyekea kwa watawala na wenye mamlaka, kuwatii na kuwa tayari kwa kila kazi njema.
\v 2 Wakumbushe kutomtendea mtu yeyoteubayawaepuke majibizano, wawape nafasi watu wengine katika kufanya maamuzi na kuonyesha unyenyekevu kwa watu wote.
\p
\v 3 Kwa kuwa hapo awali sisi pia tulikuwa na mawazo potofu na wakaidiwaasi. Tulipotoshwa na kufanywa watumwa wa tamaa na anasa mbalimbali.
\v 4 Lakini wakati ukarimu wa Mungu mwokozi wetu na upendo wake kwa wanadamu ulipoonekana,
\v 5 haikuwa kwa matendo yetu ya haki tuliyoitenda, bali alituokoa kwa neema yake. Alituokoa kwa kutuosha kwa kuzaliwa upya na kufanywa upya kwa Roho Mtakatifu.
\v 6 Mungu alimwaga Roho Mtakatifu kwa wingi juu yetu kupitia mwokozi wetu Yesu Kristo.
\v 7 Alifanya hivi ili kwamba, tukiisha kuhesabiwa haki kwa neema yake, tupate kuwa warithi wenye tumaini la uzima wa milele.
\p
\v 8 Huu ni ujumbe wa kuaminika. Ninataka myanene mambo haya, ili wale wanaomwamini Mungu wawe waangalifu katika kutenda mema. Mambo haya ni mazuri na yanafaa kwa kila mtu.
\v 9 Lakini jiepusheni na mijadala ya na nasaba, mashindano na migongano kuhusu sheria. Mambo hayo hayana faida na hayafai.
\v 10 Mkataeni yeyote anayesababisha migawanyiko kati yenuBaada ya onyo moja ama mawili,
\v 11 jueni kwamba mtu wa jinsi hiyo ameiacha njia iliyo sahihi na anatenda dhambi na kujihukumu mwenyewe.
\p
\v 12 Nitakapomtuma kwako Artema au Tikiko, harakisha uje kwangu huku Nikopoli ambapo nimeamua kukaa kipindi cha baridi.
\v 13 Fanya kila uwezalo kuwatuma Zena mwanasheria, na Apolo, pasipo kupungukiwa na kitu.
\v 14 Watu wetu lazima wajifunze kujishughulisha katika kazi nzuri ambazo zinatimiza mahitaji muhimu ili kwamba wasije wakawa wasiozaa matunda.
\p
\v 15 Wote walio pamoja nami wanakusalimu. Wasalimie wale wanaotupenda katika imani. Neema na iwe nanyi nyote.