sw_ulb/34-NAM.usfm

97 lines
7.2 KiB
Plaintext
Raw Permalink Blame History

This file contains ambiguous Unicode characters

This file contains Unicode characters that might be confused with other characters. If you think that this is intentional, you can safely ignore this warning. Use the Escape button to reveal them.

\id NAM
\ide UTF-8
\h Nahumu
\toc1 Nahumu
\toc2 Nahumu
\toc3 nam
\mt Nahumu
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Tamko kuhusu Ninawi. Kitabu cha maono ya Nahumu, Mwelkoshi.
\q1
\v 2 Yehova ni Mungu mwenye wivu na mlipiza kisasi; Yehova hulipiza kisasi na amejaa ghadhabu; Yehova ni Mungu hulipiza kisasi kwa adui zake, na huiendeleza hasira yake kwa adui zake.
\q1
\v 3 Yehova si mwepesi wa hasira na ni mwenye nguvu; hatawahesabia haki watu waovu. Yehova hufanya njia yake kwenye upepo wa kisulisuli na dhoruba, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.
\q1
\v 4 Huikemea bahari na kuifanya ikauke; hukausha mito yote. Bashani ni dhaifu, na Karmeli pia; maua ya Lebanoni imekuwa dhaifu.
\q1
\v 5 Milima hutetemeka uweponi mwake, na vilima huyeyuka; nchi huanguka mbele zake, kweli, dunia na watu wote wanaoishi ndani yake.
\q1
\v 6 Nani anaweza simama mbele ya ghadhabu yake? Nani anaweza zuia ukali wa hasira yake? Ghadhabu yake imemwagwa kama moto, na miamba ameipasua.
\q1
\v 7 Yehova ni mwema, boma katika siku ya taabu; na yeye huwatambua wale wanaomkimbilia.
\q1
\v 8 Lakini atafanya mwisho wa adui zake kwa mafuriko ya kutisha; atawawinda kwenye giza.
\q1
\v 9 Watu wanapanga nini dhidi ya Yehova? Yeye atakomesha; taabu haitainuka mara ya pili.
\q1
\v 10 Kama michongoma na kama mvinyo wa walewao, wataharibiwa kama mabua makavu.
\q1
\v 11 Kutoka kwako, Ninawi, amejitokeza mmoja ambaye alipanga uovu dhidi ya Yehova, mshauri muovu.
\v 12 Hivi ndivyo anavyosema Yehova, “Hata kama wana nguvu zao timilifu na idadi timilifu, hata hivyo wataondolewa; watu wao hawatakuwepo tena. Lakini wewe, Yuda: Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena.
\q1
\v 13 Sasa nitaivunja ile nira ya watu kutoka kwako; nitaikata minyororo yako.”
\v 14 Yehova ametoa amri juu yako, Ninawi: “Hakutakuwa na uzao tena utakaoendeleza jina lako. Nitaharibu sanamu zilizochongwa na kuziondoa sanamu za chuma kutoka kwenye nyumba za miungu yenu. Nitaandaa kaburi lako, kwa kuwa umedharauliwa.”
\q1
\v 15 Tazama, juu ya milima kuna miguu ya mtu aletaye habari njema, anayetangaza amani! Sherehekeeni sikukuu zenu, Yuda, na timizeni nadhiri zenu, kwa maana yule mwovu hatawavamia tena; ameondolewa kabisa.
\c 2
\cl Sura 2
\p
\v 1 Yule ambaye atakutawanya anakuja dhidi yako. Linda kuta za mji, linda barabara, imarisha viuno vyako, kusanya nguvu zako zote.
\v 2 Maana Yehova anarejesha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli, ingawa wateka nyara waliwaharibu na kuharibu matawi ya zabibu zao.
\v 3 Ngao za mashujaa wake ni nyekundu, na askari wamevaa nguo nyekundu; magari ya vita yanang'ara na vyuma vyake katika siku ambayo yaliandaliwa, na mikuki ya mivinje inarushwa hewani.
\q1
\v 4 Magari ya vita yanapita kasi kwenye mitaa; yanakimbia nyuma na mbele kwenye mitaa mipana. Yapo kama mienge, na yanakimbia kama umeme.
\q1
\v 5 Huwakumbuka mashujaa wake; wanajikwaa kila mmoja kwa mwingine katika kutembea kwao; wanaharakisha kuushambulia ukuta wa mji. Ngao kubwa imetayarishwa kuwakinga hawa washambuliaji.
\q1
\v 6 Malango kwenye mito yamelazimishwa kufunguka, na jumba la mfalme limeanguka.
\q1
\v 7 Huzabu amevuliwa mavazi yake na amachukuliwa; watumishi wake wa kike wanaomboleza kama njiwa, wakipiga vifua vyao.
\v 8 Ninawi ni kama bwawa la maji linalovuja, huku watu wake wakikimbia kama maji yanayotiririka. Wengine wanasema, “Simama, simama,” lakini hakuna anayegeuka nyuma.
\q1
\v 9 Chukua nyara ya fedha, chukua nyara ya dhahabu, maana hakuna mwisho wa hazina, kwa fahari ya vitu vyote vizuri vya Ninawi.
\q1
\v 10 Ninawi ipo tupu; tupu na imeharibiwa. Moyo wa kila mtu unayeyuka, magoti ya kila mmoja yanagongana pamoja, na uchungu upo kwa viuno vya kila mmoja; sura zao wote zimepauka.
\q1
\v 11 Sasa liko wapi pango la simba, sehemu ambapo wana-simba wadogo hula chakula, sehemu ambapo simba dume na simba jike walitembea, na wana-simba, ambapo hawakuogopa kitu chochote?
\q1
\v 12 Simba alirarua mawindo yake vipande vipande kwa ajili ya watoto wake; aliwanyonga mawindo wake kwa ajili ya wake zake, na kulijaza pango lake mawindo, tundu lake kwa mizoga iliyoraruliwa.
\v 13 “Tazama, mimi nipo kinyume na wewe- hili ni neno la Yehova wa majeshi. Nitayachoma magari yenu ya vita katika moshi, na upanga utameza wana-simba wenu. Nitakatilia nyara zenu kutoka kwenye nchi yenu, na sauti za wajumbe wenu hazitasikika tena.”
\c 3
\cl Sura 3
\p
\v 1 Ole kwa mji uliojaa damu! Wote umejaa uongo na mali za wizi; waadhiriwa wapo kwake daima.
\v 2 Lakini sasa kuna kelele za mijeledi na sauti za magurudumu yanayozunguka, farasi wanaokimbia, na magari ya vita yanao rukaruka.
\v 3 Wapanda farasi wanashambulia, panga zinameremeta na mikuki inang'aa, marundo ya maiti, idadi kubwa ya miili isiyohesabika- washambuliaji wanajikwaa juu yake.
\v 4 Hii inatokea kwa sababu ya matendo ya tamaa ya kahaba mrembo, mtaalam wa uchawi, mwenye kuuza mataifa kupitia kwa ukahaba wake, na watu kupitia matendo yake ya kichawi.
\q1
\v 5 “Tazama, mimi nipo kinyume na wewe --- hili ni neno la Yehova wa majeshi-- sketi yako nitaiinua juu ya uso wako na kuzionyesha sehemu zako za siri kwa mataifa, aibu yako kwa falme.
\q1
\v 6 Nitarusha uchafu wa kuchukiza kwako na kukufanya uwe mbaya sana; nitakufanya uwe mtu wa kutazamwa na kila mmoja.
\q1
\v 7 Itakuwa kwamba kila mmoja anayekutazama atakukimbia na kusema, Ninawi ameharibika; ni nani ataomboleza kwa ajili yake? Ni wapi nitampata mtu anayeweza kukufariji?”
\q1
\v 8 Ninawi, je wewe ni bora kuliko No-amoni, uliojengwa juu ya Mto Naili, uliokuwa umezungukwa na maji, ambao ulinzi wake ilikuwa bahari, na bahari ilikuwa ukuta wake?
\q1
\v 9 Ethiopia na Misri walikuwa nguvu zake, na mwisho wake haukuwepo; Putu na Libya walikuwa rafiki zake.
\q1
\v 10 Lakini No-amoni alichukuliwa; alikwenda kwenye mateka; watoto wake wadogo walivunjwa vipande vipande katika kila makao makuu ya mtaa; adui zake walipiga kura kwa watu wake wenye heshima, na wakuu wake wote walifungwa minyororo.
\q1
\v 11 Wewe pia utalewa; utajaribu kujificha, na utatafuta kimbilio kutoka kwa adui yako.
\q1
\v 12 Ngome zako zote zitakuwa kama mitini yenye tini zilizoiva mapema: kama zikitikiswa, zitaangukia ndani ya kinywa cha mlaji.
\q1
\v 13 Tazama, watu miongoni mwenu ni wanawake; malango ya nchi yako yamefunguliwa wazi kwa adui zako; moto umeharibu bawaba zake.
\q1
\v 14 Nenda ukachote maji kwa ajili ya kuzingirwa; ziimarishe ngome zako; nenda kwenye udongo na kandamiza matope; finyanga kwa ajili ya matofali.
\q1
\v 15 Moto utakuteketeza pale, na upanga utakuangamiza. Utateketezwa kama nzige wachanga wanavyoteketeza kila kitu. Ninyi wenyewe mjitengeneze kuwa wengi kama nzige wachanga, na wengi kama nzinge waliopevuka.
\v 16 Umezidisha wafanyabiashara wako zaidi kuliko nyota mbinguni; lakini wapo kama nzige wachanga; wanapora nchi na kisha kuruka kwenda zake.
\q1
\v 17 Wafalme wenu wapo kama kundi la nzige, na wakuu wenu wa majeshi ni kama nzige watuao kwenye ukuta wakati wa siku ya baridi. Lakini jua linapowaka wanaruka kwenda zao; na mahali waendapo hakuna anayepajua.
\q1
\v 18 Mfalme wa Ashuru, wachungaji wako wamelala; watawala wako wamejilaza chini kupumzika. Watu wako wametawanyika juu ya milima, na hakuna hata mmoja wa kuwakusanya.
\v 19 Hakuna uponyaji unaowezekana kwa ajili ya vidonda vyako. Vidonda vyako ni vikubwa. Kila anayesikia habari zako atapiga makofi kwa furaha juu yako. Ni nani ambaye hajaguswa na uovu wako wa daima?