\v 1 Mimi ni Paulo mtume. Mimi si mtume kutoka kwa wanadamu wala kupitia kwa mwanadamu, lakini kupitia kwa Yesu Kristo na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu.
\v 10 Kwani sasa hivi ninatafuta uthibitisho wa watu au Mungu? Ninatafuta kuwafurahisha wanadamu? Kama ninaendelea kujaribu kuwafurahisha wanadamu, mimi sio mtumishi wa Kristo.
\v 13 Mmekwisha sikia juu ya maisha yangu ya nyuma katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyokuwa nikilitesa kwa ukali kanisa la Mungu zaidi ya kipimo na kuliteketeza.
\v 2 Nilienda kwa sababu Mungu alijidhihirisha kwangu kwamba nilipaswa kwenda. Niliweka mbele yao Injili ambayo niliitangaza kwa watu wa mataifa. (Lakini niliongea kwa siri kwa waliosemekana kuwa viongozi muhimu). Nilifanya hivi ili kuhakikisha kwamba nilikuwa sikimbii, au nilikimbia bure.
\v 3 Lakini hata Tito, aliyekuwa pamoja nami, aliyekuwa Myunani, alilazimishwa kutahiriwa.
\v 4 Jambo hili lilitokea kwa sababu ya ndugu wa uongo waliokuja kwa siri kupeleleza uhuru tuliokuwa nao katika Kristo Yesu. Walitamani kutufanya sisi kuwa watumwa wa sheria.
\v 6 Lakini wale waliosemwa kuwa walikuwa viongozi hawakuchangia chochote kwangu. Chochote walichokuwa wakikifanya hakikuwa na maana kwangu. Mungu hakubali upendeleo wa wanadamu.
\v 7 Badala yake, waliniona kwamba nimeaminiwa kuitangaza injili kwa wale ambao hawakutahiriwa. Ilikuwa kama Petro atangaze injili kwa waliotahiriwa.
\v 9 Wakati Yakobo, Kefa, na Yohana, waliotambulika kuwa waliojenga Kanisa, walifahamu neema niliyopewa mimi, walitupokea katika ushirika mimi na Barnaba. Walifanya hivi ili kwamba twende kwa watu wa mataifa, na ili kwamba waweze kwenda kwa wale waliotahiriwa.
\v 12 Kabla ya watu kadhaa kuja kutoka kwa Yakobo, Kefa alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa. Lakini hawa watu walipokuja, aliacha na kuondoka kutoka kwa watu wa mataifa. Alikuwa anaogopa watu ambao walihitaji tohara.
\v 13 Vilevile Wayahudi wengine waliungana na unafiki huu pamoja na Kefa. Matokeo yake yalikuwa kwamba hata Barnaba alichukuliwa na unafiki wao.
\v 14 Lakini nilipoona kwamba walikuwa hawafuati injili ya kweli, nilimwambia Kefa mbele yao wote, “Kama ninyi ni Wayahudi lakini mnaishi tabia za watu wa mataifa badala ya tabia za Kiyahudi, kwa nini mnawalazimisha watu wa mataifa kuishi kama Wayahudi?”
\v 15 Sisi ambao ni Wayahudi kwa kuzaliwa na siyo “Watu wa mataifa wenye dhambi”
\v 16 fahamu kwamba hakuna anayehesabiwa haki kwa matendo ya sheria. Badala yake, wanahesabiwa haki kwa imani ndani ya Yesu Kristo. Tulikuja kwa imani ndani ya Kristo Yesu ili kwamba tunahesabiwa haki kwa imani ndani ya Kristo na siyo kwa matendo ya sheria. Kwa matendo ya sheria hakuna mwili utakao hesabiwa haki.
\v 17 Lakini kama tunapomtafuta Mungu kwa kutuhesabia haki ndani ya Kristo, tunajikuta wenyewe pia kuwa wenye dhambi, je Kristo alifanywa mtumwa wa dhambi? Siyo hivyo!
\p
\v 18 Maana kama nikijenga tegemeo langu juu ya kutunza sheria, tegemeo ambalo nilikwisha liondoa, najionesha mwenyewe kuwa mvunja sheria.
\v 20 Nimesulubiwa pamoja na Kristo. Si mimi tena ninayeishi, bali Kristo anaishi ndani yangu. Maisha ninayoishi katika mwili ninaishi kwa imani ndani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda na akajitoa kwa ajili yangu.
\v 6 Abrahamu “Alimwamini Mungu akahesabiwa kuwa mwenye haki.”
\v 7 Kwa namna ile ile eleweni kwamba, wale ambao wanaamini ni watoto wa Abrahamu.
\v 8 Andiko lilitabiri kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa mataifa kwa njia ya imani. Injili ilihubiriwa kwanza kwa Abrahamu: “katika wewe mataifa yote yatabarikiwa.”
\v 10 Wale ambao wanategemea matendo ya sheria wako chini ya laana. Kwa kuwa imeandikwa, “Amelaaniwa kila mtu ambaye hashikamani na mambo yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria, kuyatenda yote.”
\v 11 Sasa ni wazi kwamba Mungu hamhesabii haki hata mmoja kwa sheria, kwa kuwa “Mwenye haki ataishi kwa imani.”
\v 12 Sheria haitokani na imani, lakini badala yake “Ambaye hufanya mambo haya katika sheria, ataishi kwa sheria.”
\p
\v 13 Kristo alitukomboa sisi kutoka katika laana ya sheria wakati alipofanyika laana kwa ajili yetu. Kwa kuwa imeandikwa, “Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti.”
\v 14 Lengo lilikuwa kwamba, baraka ambazo zilikuwa kwa Abrahamu zingekuja kwa watu wa mataifa katika Kristo Yesu, ili kwamba tuweze kupokea ahadi ya Roho kupitia imani.
\p
\v 15 Ndugu, ninazungumza kwa namna ya kibinadamu. Hata wakati ambapo agano la kibinadamu limekwisha kuwekwa imara, hakuna awezaye kupuuza au kuongezea.
\v 16 Sasa ahadi zilisemwa kwa Abrahamu na kwa kizazi chake. Haisemi, “kwa vizazi,” kumaanisha wengi, bali badala yake kwa mmoja pekee, “kwa kizazi chako,” ambaye ni Kristo.
\v 17 Sasa nasema hivi, sheria ambayo ilikuja miaka 430 baadaye, haiondoi agano la nyuma lililowekwa na Mungu.
\v 18 Kwa kuwa kama urithi ungelikuja kwa njia ya sheria, usingekuwa tena umekuja kwa njia ya ahadi. Lakini Mungu aliutoa bure kwa Abrahamu kwa njia ya ahadi.
\p
\v 19 Kwa nini sasa sheria ilitolewa? Iliongezwa kwa sababu ya makosa, mpaka mzao wa Abrahamu aje kwa wale ambao kwao alikuwa ameahidiwa. Sheria iliwekwa katika shinikizo kupitia malaika kwa mkono wa mpatanishi.
\v 21 Kwa hiyo je sheria iko kinyume na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa kuwa kama sheria iliyokuwa imetolewa ilikuwa na uwezo wa kuleta uzima, haki ingepatikana kwa sheria.
\v 22 Lakini badala yake, andiko limefunga mambo yote chini ya dhambi. Mungu alifanya hivi ili kwamba ahadi yake ya kutuokoa sisi kwa imani katika Yesu Kristo iweze kupatikana kwa wale wanao amini.
\v 9 Lakini sasa kwamba mnamjua Mungu, au kwamba mnajulikana na Mungu, kwa nini mnarudi tena kwenye kanuni dhaifu za kwanza na zisizo za thamani? Je mnataka kuwa watumwa tena?
\v 14 Ingawa hali yangu ya mwili iliwaweka katika jaribu, hamkunidharau au kunikataa. Badala yake mlinipokea kama malaika wa Mungu, kana kwamba nilikuwa Kristo Yesu mwenyewe.
\v 24 Mambo haya yanaweza kuelezwa kwa kutumia mfano, kwa kuwa wanawake hawa wanafanana na maagano mawili. Mojawapo kutoka katika mlima Sinai. Huzaa watoto ambao ni watumwa. Huyu ni Hajiri.
\v 26 Bali Yerusalemu ambayo iko juu ni huru, na hii ndiyo mama yetu.
\v 27 Kwa kuwa imeandikwa, “Furahi, wewe mwanamke uliye tasa, wewe usiye zaa. Paza sauti na upige kelele kwa furaha, wewe ambaye huna uzoefu wa kuzaa. Kwa maana wengi ni watoto wa aliye tasa, zaidi ya wale wa yule ambaye ana mume.”
\p
\v 28 Sasa ndugu, kama Isaka, ninyi ni watoto wa ahadi.
\v 30 Maandiko husemaje? “Muondoe mwanamke mtumwa pamoja na mwanawe wa kiume. Kwa kuwa mtoto wa mwanamke mtumwa hatarithi pamoja na mtoto wa mwanamke huru.”
\v 10 Nina matumaini na ninyi katika Bwana kwamba hamtafikiri kwa njia nyingine yoyote. Yeyote yule atakayewapotosha atabeba hukumu yake yeye mwenyewe, yeyote yule.
\v 16 Nasema, tembeeni kwa roho, na wala hamtazitimiza tamaa za mwili.
\v 17 Kwa kuwa mwili una tamaa kubwa dhidi ya Roho, na Roho ina tamaa kubwa dhidi ya mwili. Hizi zinapingana kila moja na nyingine. Matokeo ni kwamba hamfanyi vitu mnavyotamani kuvifanya.
\v 21 Wivu, ulevi, ulafi na mambo mengine kama haya. Nawaonya ninyi, kama nilivyowaonya mwanzoni, kwamba wale wanaofanya mambo kama hayo hawataurithi ufalme wa Mungu.
\v 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani,
\v 23 upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo.
\v 1 Ndugu, ikiwa mtu amekamatwa katika uovu, ninyi mlio wa kiroho, mnawiwa kumrejesha huyo ndugu katika roho ya upole. Huku mkijiangalia wenyewe ili msijaribiwe.
\v 8 Kila apandaye mbegu katika asili yake ya dhambi atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye mbegu katika Roho, atavuna uzima wa milele kutoka kwa Roho.
\v 11 Angalieni ukubwa wa barua nilizowaandikia kwa mkono wangu mwenyewe.
\v 12 Wale wanaotaka kufanya mema kwa mtazamo wa mwili ndiyo wenye kuwalazimisha mtahiriwe. Wanafanya hivyo kwa sababu wasiingie kwenye mateso ya msalaba wa Kristo.