\v 1 Kile tulichokiona tangu mwanzo, kile tulichokisikia, kile tulichokiona kwa macho yetu, kile tulichokitazama, na mikono yetu imekishika kuhusu Neno la uzima.
\v 2 Na ule uzima ulifanywa kujulikana wazi na tumeuona, na kuushuhudia, na kuwatangazia uzima wa milele, ambao ulikuwako kwa Baba na ulifanywa kujulikana kwetu.
\v 3 Kile tulichokiona na kukisikia twakitangaza kwenu, ili kwamba muweze kujumuika pamoja nasi, na ushirika wetu pamoja na Baba na Mwanae Yesu Kristo.
\v 4 Na tunawaandikia mambo haya ninyi ili kwamba furaha yetu iwe timilifu.
\p
\v 5 Huu ndio ujumbe tuliousikia kutoka kwake na kuwatangazia ya kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hakuna giza hata kidogo.
\v 6 Kama tukisema kwamba tunaushirika naye na twatembea gizani, twadanganya na hatutendi kweli.
\v 7 Lakini tukitembea katika nuru kama alivyo yeye nuruni, Twashirikiana sisi kwa sisi, na damu ya Yesu Kristo, mwanae yatutakasa kutoka dhambini.
\v 8 Kama tukisema hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, na kweli haimo ndani yetu.
\v 9 Lakini tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na haki kutusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.
\v 1 Watoto wangu wapendwa, nawaandikia mambo haya kwenu ili msitende dhambi. Lakini kama mmoja wenu akitenda dhambi, tunaye wakili aliye pamoja na Baba, Yesu Kristo- ambaye ni mwenye haki.
\v 2 Yeye ni mpatanishi kwa dhambi zetu, na si kwa dhambi zetu pekee, lakini pia kwa ulimwengu mzima.
\v 12 Nawaandikia ninyi, watoto wapendwa, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu kwa ajili ya jina lake.
\v 13 Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mnamjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mnamjua Baba.
\v 14 Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mnamjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mko na nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, na mmemshinda yule mwovu.
\p
\v 15 Msiipende dunia wala vitu ambavyo vimo katika dunia. Iwapo yule ataipenda dunia, upendo wa kumpenda Baba haumo ndani yake.
\v 16 Kwani kila kitu kilichomo katika dunia- tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha uzima- havitokani na Baba lakini vinatokana na dunia.
\v 18 Watoto wadogo, ni wakati wa mwisho. Kama ambavyo mmesikia kwamba mpinga kristo anakuja, hata sasa wapinga kristo wameshakuja, kwa hali hii tunajua kwamba ni wakati wa mwisho.
\v 19 Waliondoka zao kutoka kwetu, kwani hawakuwa wa kwetu. Kama vile wangekuwa wa kwetu wangeendelea kuwa pamoja nasi. Lakini wakati walipo kwenda zao, hicho kilionyesha hawakuwa wa kwetu.
\v 20 Lakini ninyi mmetiwa mafuta kutoka kwa yule Mtakatifu, nanyi nyote mnajua kweli.
\v 21 Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamujui ukweli, bali kwa sababu mnaijua na kwa sababu hakuna uongo wa ile kweli
\v 22 Nani ni mwongo bali ni yeye anayepinga kwamba Yesu ni Kristo? Huyu mtu ni mpinga kristo, pale anapo mpinga Baba na Mwana.
\v 24 Kama kwa ajili yenu, kile mlichosikia toka mwanzo acha kiendelee kuwa ndani yenu. Kama kile mlichosikia toka mwanzo kitakaa ndani yenu, pia, mtakaa ndani ya Mwana na Baba.
\v 25 Na hii ni ahadi aliyotupatia sisi: uzima wa milele.
\v 27 Na kwa ajili yenu, yale mafuta mliyoyapokea kutoka kwake yanakaa ndani yenu, na hamtahitaji mtu yeyote kuwafundisha. Bali kama mafuta yake yanawafundisha kuhusu mambo yote na ni kweli na siyo uongo, na hata kama yameshawafundisha, kaeni ndani yake.
\p
\v 28 Na sasa, watoto wapendwa, kaeni ndani yake, ili wakati atakapotokea, tuweze kuwa na ujasiri na siyo kujisikia aibu mbele yake katika kuja kwake.
\v 1 Oneni ni pendo la namna gani ametupatia Baba, kwamba tunaitwa watoto wa Mungu, na hivi ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui kwa kuwa haukumtambua yeye.
\v 2 Wapendwa sisi sasa ni watoto wa Mungu, na haijadhihirika bado jinsi tutakavyokuwa. Twajua kwamba Kristo atakapoonekana, tutafanana naye, kwani tutamuona kama alivyo.
\v 8 Atendaye dhambi ni wa ibilisi, kwa sababu ibilisi ni mtenda dhambi tangu mwanzo. Kwa sababu hii Mwana wa Mungu alidhihilishwa ili aweze kuziharibu kazi za ibilisi.
\v 9 Yeyote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu mbegu ya Mungu hukaa ndani yake. Hawezi kuendelea kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu.
\v 10 Katika hili watoto wa Mungu na watoto wa ibilisi wanafahamika. Yeyote asiyetenda kilicho cha haki, siyo wa Mungu, wala yule ambaye hawezi kumpenda ndugu yake.
\v 12 siyo kama Kaini ambaye alikuwa wa mwovu na alimuua ndugu yake. Na kwa nini alimuua? Kwa sababu matendo yake yalikuwa maovu, na yale ya ndugu yake yalikuwa ya haki.
\v 16 Katika hili tunalijua pendo, kwa sababu kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Nasi yatupasa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu.
\v 17 Lakini yeyote aliye na vitu, na anamuona ndugu yake mwenye uhitaji, lakini huuzuia moyo wake wa huruma kwa ajili yake; je, upendo wa Mungu unakaaje ndani yake?
\v 6 Sisi ni wa Mungu. Yeye amjuaye Mungu hutusikiliza sisi. Yeye asiye wa Mungu hawezi kutusikiliza. Katika hili tunajua roho wa kweli na roho wa uongo.
\v 7 Wapendwa, tupendane sisi kwa sisi, kwa vile upendo hutoka kwa Mungu, na kila mmoja apendaye amezaliwa na Mungu na kumjua Mungu.
\v 8 Mtu asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni upendo.
\v 9 Katika hili pendo la Mungu lilifunuliwa miongoni mwetu, kwamba Mungu alimtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni ili tuishi kupitia yeye.
\v 10 Katika hili pendo, si kwamba tulimpenda Mungu, lakini yeye alitupenda, na akamtuma Mwanawe awe fidia kwa ajili ya dhambi zetu.
\v 11 Wapendwa, ikiwa Mungu alitupenda sisi, vile vile tunapaswa kupendana sisi kwa sisi.
\p
\v 12 Hakuna hata mmoja aliyemuona Mungu. Kama tukipendana sisi kwa sisi, Mungu anakaa ndani yetu na upendo wake umekamilika ndani yetu.
\v 13 Katika hili tunajua kuwa tunakaa ndani yake na yeye ndani yetu, kwa sababu ametupa Roho wake.
\v 14 Tena, sisi tumeonana na kushuhudia kuwa Baba amemtuma Mwana kuwa mwokozi wa ulimwengu.
\v 15 Kila anayekiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu anakaa ndani yake na yeye ndani ya Mungu.
\v 16 Tena tumejua na kuamini upendo alio nao Mungu kwa ajili yetu. Mungu ni pendo, na yeye anayekaa ndani ya upendo anakaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.
\v 17 Kwa sababu hii, upendo huu umekwisha kukamilika katikati yetu, ili tuwe na ujasiri siku ya hukumu, kwa sababu kama yeye alivyo, na sisi ndivyo tulivyo katika ulimwenngu huu.
\v 18 Hakuna hofu ndani ya pendo. Lakini pendo kamili huitupa hofu nje, kwa sababu hofu huhusiana na hukumu. Lakini yeye aogopaye hajakamilishwa katika pendo.
\v 19 Tunapenda kwa sababu Mungu alitupenda kwanza.
\v 20 Ikiwa mmoja atasema, “Nampenda Mungu” lakini hawezi kumpenda ndugu yake, ni mwongo. Kwa sababu asiyempenda ndugu yake, anayemuona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamuona.
\v 1 Yeyote anayeamini kuwa Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na yeyote ampendaye yeye ambaye ametoka kwa Baba pia huwapenda watoto wake.
\v 2 Kwa hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu -- tunapompenda Mungu na kutii amri zake.
\v 3 Hivi ndivyo tunavyompenda Mungu kwamba twazitii amri zake. Na amri zake ni nyepesi.
\v 4 Kwa kuwa kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Na huu ndio ushindi wa kuushinda ulimwengu, hata imani yetu.
\v 5 Ni nani aushindaye ulimwengu? Ni yule aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.
\p
\v 6 Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu- Yesu Kristo. Hakuja tu kwa maji bali kwa maji na damu.
\v 7 Kwa kuwa kuna watatu washuhudiao:
\v 8 Roho, maji na damu. Hawa watatu hukubaliana. \f + \ft Zingatia: Maneno haya “Baba, Neno, na Roho Mtakatifu” hayaonekani katika nakala bora za kale. \f*
\v 9 Kama tunaupokea ushuhuda wa wanadamu ushuhuda wa Mungu ni mkuu kuliko huo. Kwa kuwa ushuhuda wa Mungu ni huu- kwamba anao ushuhuda kuhusiana na Mwanawe.
\v 10 Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu ana ushuhuda ndani yake mwenyewe. Na yeyote asiye mwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini ushuhuda ambao Mungu ameuleta kuhusu Mwanawe.
\v 16 Kama mtu amwonaye ndugu yake anatenda dhambi isiyopelekea kifo, yampasa kuomba na Mungu atampa uzima. Ninasema kwa wale ambao dhambi yao ni ile isiyopelekea kifo. Kuna dhambi ipelekeayo kifo; sisemi kwamba anapaswa kuomba kwa ajilli ya dhambi hiyo.
\v 17 Matendo yote yasiyo ya haki ni dhambi, lakini kuna dhambi isiyopelekea kifo.
\v 18 Tunajua ya kuwa aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi. Bali aliyezaliwa na Mungu hutunzwa naye salama daima, na yule mwovu hawezi kumdhuru.
\v 20 Lakini twajua kwamba Mwana wa Mungu amekuja na ametupatia ujuzi, kwamba tunamjua yeye aliye kweli na kwamba tumo ndani yake yeye aliye kweli, hata katika Mwanawe Yesu Kristo. Ni Mungu wa kweli na uzima wa milele.